airport jogging

mavazi

aus521

aus9

Tuesday, January 16, 2018

MAMBOSASA: BAADHI YA WAFUNGWA WALIOACHIWA NA JPM WANAFUKUA SILAHA ZAO

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limedai kuwa linazo taarifa kwamba baadhi ya wahalifu walioachiwa kwa msamaha wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli wameanza kufukua silaha zao walizokuwa wamezificha ili zifanye kazi ya uhalifu katika maeneo mbalimbali huku akisema hawatasita kuwarudisha tena jela iwapo wataendelea na tabia za uhalifu.

WATUHUMIWA WA UGAIDI ARUSHA WAVUA NGUO MAHAKAMANI

WATUHUMIWA katika kesi ya matukio mbalimbali ya ugaidi mkoani Arusha, Leo January 16, 2018 wamevua nguo na kubaki utupu wakati wakishushwa kwenye basi la Magereza la Kisongo walipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kusomewa mashtaka yanayowakabili.

MABINTI WA CHIBOK WALIOTEKWA NA BOKO HARAM WAGOMA KURUDI NYUMBANI

Kundi la Boko Haram limetoa video mpya ikionyesha wasichana 14 waliotekwa katika mji wa Chibok, Kaskazini mwa Nigeria mnamo mwezi Aprili 2014 ambapo katika video hiyo wamesema kamwe hawatarejea nyumbani kwa sababu sehemu wanayoishi sasa ni takatifu na wanapata kila wanachohitaji.

Mabinti 300 wa Shule ya Chibok walitekwa na kundi la kigaidi la Boko Haram mwaka 2014 ambapo baadhi yao walifanikiwa kutoroka licha ya wenzao kubaki na hawajulikani walipo. Kumekuwa na picha na video ambazo Boko Haram huzitoa mara chache ili kuwaumiza wazazi wao.
Kundi hilo limekuwa maarufu katika ukanda wa Afrika Magharibi kufanya vitendo vya kihalifu ikiwemo mauaji ya kinyama miongoni mwa raia. Inasemekana mabinti hao wanawatumikisha kingono.

Muigizaji wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’. Muigizaji wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amepata pigo kwa kuondokewa na mama yake mzazi. Mungu ailaze roho ya mama Johari mahala pema peponi, Amina.

Muigizaji wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
Muigizaji wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amepata pigo kwa kuondokewa na mama yake mzazi. Mungu ailaze roho ya mama Johari mahala pema peponi, Amina.

Sabrina Rupia ‘Cathy’. MKONGWE wa sinema za Kibongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ ameamua kutupa sanaa kule kisha kujiweka pembeni kwa kile alichosema kwamba, hailipi na amejikita zaidi kwenye kuuza chakula. Cathy aliiambia Za Motomoto News kuwa, kwa sasa amejikita kwenye kupika vyakula ambavyo anasambaza sehemu mbalimbali anapopata oda na imekuwa ikimlipa tofauti na filamu hivyo ameiweka sanaa pembeni kwanza maana kazi ya kupika haina umri na wala haimtupi mtu. “Kupika na kuuza chakula sasa hivi ndiyo habari ya mjini, kwa sasa akili na nguvu zangu zote nimezielekeza kwenye kazi hii ya kupika maana maisha ni magumu sana nikitegemea sanaa tu na nina watoto nitafeli,” alisema Cathy.

Sabrina Rupia ‘Cathy’.
MKONGWE wa sinema za Kibongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ ameamua kutupa sanaa kule kisha kujiweka pembeni kwa kile alichosema kwamba, hailipi na amejikita zaidi kwenye kuuza chakula.

Cathy aliiambia Za Motomoto News kuwa, kwa sasa amejikita kwenye kupika vyakula ambavyo anasambaza sehemu mbalimbali anapopata oda na imekuwa ikimlipa tofauti na filamu hivyo ameiweka sanaa pembeni kwanza maana kazi ya kupika haina umri na wala haimtupi mtu.

“Kupika na kuuza chakula sasa hivi ndiyo habari ya mjini, kwa sasa akili na nguvu zangu zote nimezielekeza kwenye kazi hii ya kupika maana maisha ni magumu sana nikitegemea sanaa tu na nina watoto nitafeli,” alisema Cathy.

Tuesday, October 31, 2017

Joti kawajibu wanaomsema kwa kunyoa kiduku kwenye harusi yake



Jumamosi iliyopita ilikua harusi ya Mchekeshaji maarufu Tanzania Lucas Muhavile maarufu kama Joti ambapo gumzo lilikua pia nywele zake alizonyoa kwa staili ya kiduku na kuingia nacho Kanisani jambo ambalo lilifanya baadhi ya watu kuongea sana kwenye mitandao.
Jana AyoTV na millardayo.com zinae Joti kwenye Exclusive Interview ambapo amewajibu waliomsema kuhusu kiduku chake, >>> “Sidhani kama kuna sheria au kuna maandiko yameandika kwamba ukinyoa hivi hutakiwi kufunga ndoa, hii sanasana iko kwenye maadili tu
“Nilimuomba Padri na akanielewa na kuniambia wewe ni Msanii tunajua cha kufanya usisuke tu, fumua hizo nywele ziwe tu kawaida zibanebane vizuri”

“Hawapumui na wakipumua wanapumulia gerezani” – Rais Magufuli.





Hii kauli inatoka kwenye siku ya kwanza ya ziara ya siku mbili ya Rais Magufuli Mwanza, amehutubia Wananchi kwenye viwanja vya Mwatex Nyakato na moja ya nukuu za kauli zake ni hii ya “siku hizi hawapumui na wakipumua wanapumulia gerezani” tazama hii video hapa chini kupata yote mengine aliyoyasema Mr. President

BREAKING NEWS

Habari zilizotufikia muda huu ni kwamba Mbunge wa Kigoma Mjini ambae pia ni kiongozi wa chama cha ACT WAZALENDO Zitto Kabwe amekamatwa na polisi.



Taarifa zaidi zinasema Zitto amekamatwa akiwa nyumbani kwake Dar es salaam na kupelekwa kituo cha Polisi Chang’ombe, habari hii imethibitishwa na Afisa Habari wa ACT Wazalendo Abdallah Khamis ambaye ameeleza kuwa sababu za kukamatwa kwake ni hotuba aliyoitoa juzi katika kata ya Kijichi.

Wednesday, January 4, 2017

HIKI ndicho kilichovunja ndoa ya Mkwasa na TFF



TFF limesema, kuachana na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Charles Boniface Mkwassa “Master” ni makubaliano ya kimkataba kwa pande zote mbili na hakukuwa na tofauti zozote ziliyojitokeza.

Afisa habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfred Lucas amesema, wanatarajia kumalizana kabisa na Mkwasa mpaka ifikapo mwezi wa Machi mwaka huu ikiwemo fidia za kukatisha mkataba.

MAX 'Mimi Nitaacha Kutoa Machozi Kwa Ajili ya Young Dee, Anguko la Pili Huwa Mara Dufu ya Anguko la Kwanza'


Meneja wa Young Dee na Mmiliki wa Studio za Authentic siku yakuzaliwa kwa Young Dee aliandika Haya kwa Uchungu akiashiria kuwa Msanii wake huyo ameanza kupotea tena kwenye Madawa ya kulevya baada ya kuhaidi kuacha:

RAPPER Feature auanza mwaka mpya kwa style ya Wema Sepetu



Rapper wa Marekani, Future ameamua kuuanza mwaka mpya wa 2017 kwa kufuta picha zote kwenye mtandao wa Instagram.

Akaunti ya rapper huyo ina followers wapatao milioni 8.7 huku akiwa amemfollow mtu mmoja pekee ambaye ni Dj Esco.


Future anaungana na malkia wa filamu Bongo, Wema Sepetu ambaye na yeye aliamua kuuanza mwaka kwa kitendo kama hicho cha kufuta picha zake kwenye mtandao huo

MWANAMUZIKI Darassa Afunguka "Diamond Hapaswi Kujiita Simba"


Msanii wa bongo fleva Darasa ameweka wazi ule mstari wake wa "sio simba, sio chui, sio mamba" kwa kusema Diamond hakupaswa kujiita simba kwani simba ni mnyama ambaye anaweza kuuliwa anapozidiwa nguvu.

40 Ya Mdogo Wa Tiffah Usipime, Mastaa Wakubwa Afrika Watajwa Kuhudhuria


STORI: GABRIEL NG’OSHA, GAZETI LA UWAZI, TOLEO 1021, JANUARI 3-9, 2017

DAR ES SALAAM: Habari ya motomoto inaeleza kuwa Januari 16, mwaka huu ndiyo siku ambayo mtoto wa kiume wa staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Nillan Nasibu ‘Chibu Junior’ atatimiza siku 40 tangu alipozaliwa Desemba 6, mwaka jana.

NAY ataja tofauti ya Diamond na Alikiba


Rapa Nay wa Mitego amefunguka na kuweka wazi kuwa katika wanamuziki watatu wakubwa Tanzania wazuri kwake yeye Alikiba atakuwa namba moja ila katika wanamuziki wakubwa watatu wafanyabiashara basi Diamond Platnumz atakuwa namba moja.Nay ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Sijiwezi', amesema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo cha EATV na kusema siku zote yeye amekuwa akimkubali sana Alikiba ingawa anatambua wazi mtaani kuna tetesi kuwa hawezi kufanya naye kazi kutokana na yeye kuwa na uswahiba

MTU mmoja amenusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa risasi na askari wa wanyamapori Sumbawanga


Mtu mmoja amenusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa risasi na kujeruhiwa mguu wa kulia na askari wa wanyamapori wa pori la Akiba la Uwanda kwa madai kuwa alikatisha kwenye hifadhi kinyume cha sheria.

MAGUFULI Awashangaa Kagera: UKIMWI nyie, Tetemeko Nyie, Mna mto Unaitwa Ngono na Kijiji cha Katerero


Magufuli amesema Kagera haipaswi kuwa ya matatizo bali ya mfano na kutolea mfano majanga yaliyotokea Kagera ya Ukimwi na tetemeko.
Pia akawaambia anajua wana kijiji kinaitwa Katerero na mto unaitwa Ngono.

POLISI kufukua kaburi la binti aliyezikwa kwa siri Arusha


Familia moja  jijini Arusha inadaiwa kumzika kwa siri mtoto wao mdogo wa kike wa miaka mitatu katika kaburi lililofichwa, huku majirani wakidanganywa kuwa binti huyo yupo hai.

Tuesday, January 3, 2017


Mashabiki wamlilia Young Dee baada ya meneja kudai amerudia tena unga

Kwa mujibu wa meneja wa Young Dee, Maximillian Rioba, rapper huyo amerejea tena kwenye matumizi ya dawa za kulevya.

Young Dee akiwa na meneja wake Max mwanzilishi wa label ya MDB
Taarifa hiyo imekuja katika wakati ambao mashabiki wengi wa muziki waliamini kuwa rapper huyo ameachana na matumizi ya unga, kama alivyoahidi mwaka uliopita alipozungumza na waandishi wa habari.

BEN SELENGO anaendelea vizuri baada ya kupata ajari mbaya.......

Msanii wa filamu Ben Selengo baada ya kupata ajali ambaya siku ya sikukuu ya Christmas na kulazwa katika Muhimbili, ameruhusiwa na sasa hivi yupo nyumbani.

Mchekeshaji huyo amedai licha ya kuwa ameruhusiwa kutoka hospital lakini bado afya yake haijakaa sawa na anahitaji maombi.
“Bado nahitaji maombi yenu wadau,” aliandika Ben Instagram “nimetoka Muhimbili nipo home ila kiafya bado,”

Hili ni gari ambalo alipata nayo ajali

Vanessa Mdee aingia studio kurekodi ngoma na rapper Tay Grin wa Malawi

Vanessa Mdee alitumbuiza kwenye show ya mkesha wa mwaka mpya nchini Malawi, mwishoni mwa wiki. Lakini hakuishia tu kutumbuiza, bali alitumia muda huo kurekodi wimbo anaoshirikishwa na rapper wa nchini humo, Tay Grin.

Vanessa Mdee akiingiza sauti kwenye booth
Kwa muda mrefu Tay alikuwa akidai kuwa anapenda aje arekodi wimbo na muimbaji huyo wa Cash Madame, na sasa fursa hiyo imepatikana hatimaye.

Mkulima aliyechomwa mkuki arejea nyumbani

Wiki iliyopita kulikuwa na habari iliyowashtua watu kwa namna moja au nyingine. Ni habari ya mkulima na mkazi wa kitongoji cha Upangwani, kijiji cha Dodoma Isanga, Kata ya Masanze, Kilosa mkoani Morogoro ,Augustino Mtitu(35), aliyechomwa mkuki mdomoni. Hatimaye kijana huyo ameruhusiwa kutoka hospitali alikokuwa amelazwa na kurejea nyumbani.

Madaktari wamesema kuruhusiwa kwa mgonjwa huyo kumetokana na yeye kupona kufuatia kufanyiwa

Karrueche awagombanisha Chris Brown na Soulja Boy

Mwaka 2017 umeanza vibaya kwa Chris Brown na Soulja Boy – kwakuwa wameanzisha bifu chanzo kikiwa ni mrembo Karrueche Tran.

Tangu alipoachana na Karrueche Chris amekuwa akimfuatilia mrembo huyo huku mara kadhaa akigombana na wanaume ambao wanaomtolea udenda. Na sasa balaa limemkumba rapper Soulja Boy baada ya kulike picha ya mrembo huyo kwenye mtandao wa Instagram kitendo ambacho kimeonekana kumkera Brown.
Soulja Boy amefunguka kupitia mtandao wa Twitter kuwa Chris amemtafuta na kumpiga mikwara baada ya kulike picha hiyo

Majambazi yapora mamilioni mbele ya askari polisi Dar


 


WATU wanaodaiwa majambazi wamepora kiasi cha fedha kinachokadiriwa kuwa zaidi ya shilingi milioni 25 katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere, eneo la Tazara, Dar es Salaam.
Gazeti hili lilishuhudia tukio hilo jana, saa 4 asubuhi wakati gari hilo likiwa kwenye foleni ya magari eneo hilo la taa za Tazara.
Watu hao wameporwa katika eneo ambalo huwa askari doria wametanda,

Nyingine ya Nikki Mbishi, Feza Kessy kuhusu hali ya Nando wa Big Brother Africa #TheChase

Siku chache baada ya kuandika message yake kuhusu afya ya rapa Chid Benz ambaye ameathirika na matumizi ya dawa za kulevya ambazo inaelezwa amekuwa akizitumia kwa muda mrefu pamoja na kupelekwa Rehab lakini bado amerudia tena, nimekutana hii nyingine ya Nikki Mbishi kuhusu Nando, mshiriki wa “BBA The Chase”.

Tuesday, November 29, 2016

katika kueleke akilele cha maadhimisho ya miaka100 ya skauti tanzania na afrika...

tsa kushilikiana na skauti kutoka poland wafanya semina inyohusu msuala ya IT(mawasiliano).
skauti kutoka poland wamkutana na skauti wa tanzania katika semina mahususi ambayo inahusiana na masuasala ya mawasiliano juu ya upokeaji, kutangaza, kutengeneza, na kuunda taarifa juu ya masuala ya mawasiliano.











Tuesday, June 7, 2016

Chuchu Hans adaiwa kunasa ujauzito


Chuchu-HansChuchu Hans.
IMELDA MTEMA
STAA wa filamu Bongo, Chuchu Hans anadaiwa kunasa ujauzito wa mchumba wake ambaye naye ni staa wa filamu, Vincent Kigosi ‘Ray’. Kwa mujibu wa chanzo ambacho kipo karibu na wawili hao, Chuchu kwa sasa ni mtu wa kujifungia ndani na amekuwa hapatikani kwenye matukio mbalimbali yanayomhusu. “Ameshanasa, tena ujauzito huo ni wa Ray, unaambiwa sasa hivi kawa mtu wa kujifungia ndani tu na kitumbo kimeshamtoka,” kilisema chanzo.
CHUCHU789111           Chuchu na Ray
Alipotafutwa Chuchu kujua ukweli alijibu; “Nashangaa, watu wengi wananifikiria hivyo lakini sitaki kuongea chochote. Labda watakuwa na husda tu ndiyo maana wananifikiria hivi,” alisema Chuchu. Ray alipotafutwa kwa njia ya simu ili kusikia kauli yake hakupokea

Esha ‘alia’ wivu kwa hausigeli wake


ESHA35GLADNESS MALLYA
S TAA wa filamu za Kibongo, Esha Buheti ‘amelia’ wivu kwa mfanyakazi wake wa ndani (hausigeli) kuwa katika maisha yake ya ndoa hapendi kumwachia ampikie mumewe kwani siyo maadili.
Akizungumza na Showbiz Xtra Esha alisema kuwa, hata mumewe akipikiwa na dada wa kazi huwa anajua kwani akikionja chakula tu lazima aulize mpishi ni nani kutokana kuwa na ladha ya tofauti. “Simwachii dada ampikie mume wangu, chakula chake napika mwenyewe labda niwe naumwa,” alisema Esha

Daktari: Diamond Anamuua Baba’ke!


BABADBaba mzazi wa Diamond, Mzee Abdul Juma.
Mwandishi wetu, Amani
DAR ES SALAAM:  “Msongo wa mawazo ni tatizo kubwa duniani linalotokana na kusheheni kwa mawazo ya kila wakati, husasan kuhusu maisha au afya. Kwa hiyo anachofanya Diamond kwa baba yake ni sawa na kumuua kwa sababu ya kumsababishia msongo,” ndivyo alivyosema daktari Rweyemamu wa hospitali moja ya jijini Dar.
Daktari Rweyemamu alizungumza na Amani hivi karibuni kufuatia habari zinazoandikwa na Magazeti Pendwa ya Global Publishers kuhusu nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwamba amemtelekeza baba yake, Abdul Juma.
Diamond-PlatnumzMsanii Diamond Platinumz
AZUNGUMZIA HISTORIA
“Nimekuwa nikisoma habari mbalimbali kwenye Magazeti Pendwa ya Global, lakini hili la Diamond kumtelekeza baba yake mimi naona lina mapana yake. Najua utetezi wa Diamond ni kwamba, baba alimtelekeza mama yake (Sanura Kasim) yeye akiwa mtoto.
“Kwa hiyo malezi yote, ameyapata kwa mama mpaka kufika kwenye kiwango cha mafanikio. Lakini pia nimewahi kusoma kwamba, baba aliomba msamaha yaishe, atambulike kama baba lakini mtoto akagoma.”

Tukio la Ajabu Kaburini

kaburi

DAR ES SALAAM! Wakazi wa Mbagala Chalambe jijini Dar es Salaam, waliamka asubuhi na kukutana na tukio lililojaa maswali mengi huku majibu yakiwa haba kufuatia kukuta kitu kaburini kikiwa kimeviringishiwa sanda.
ILIVYOKUWA
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo lilijiri hivi karibuni kwenye Makaburi ya Chalambe ambapo wakazi hao walilizunguka kaburi hilo huku wakidai kuwa, ndani ya sanda hiyo kulikuwa na mtoto aliyeuawa na kuwekwa hapo.
SHUHUDA ATOA
MAWAZO YAKE
“Jamani humu kwenye sanda kuna maiti ya mtoto mdogo. Lazima kuna mahali ameuawa, wakamviringishia sanda maskini wa Mungu, wakaja kumuweka hapa,” alisema mkazi mmoja akiwa amejikunyata baada ya kutoka kulala.
IMG-20160522-WA0001MTAZAMO WA WENGINE
Wengine walisikika wakisema kuwa, kwa vyovyote mtu au watu waliotupa kitu hicho walikuwa katika harakati za ushirikina kutokana na maelekezo ya mganga.
“Huu ni ushirikina mkubwa, lazima watu wamefanya hivi kwa maelekezo ya mganga. Huwezi kuja kutupa vitu vya uchawi kwenye kaburi la mtu, watu hawana hata woga wala hawamuogopi Mungu,” alisema mama mmoja.