habari toka grobal publisher
MATESO! Mtoto aitwaye Chacha Robert (15), (pichani), mkazi wa Musoma, Mara anateseka na ugonjwa wa ajabu wa kuota magamba kama ya nyoka sehemu ya mwili hali inayomsababishia kutengwa na jamii.Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu na familia yake zinaeleza kuwa, Chacha alizaliwa hivyo na mama yake mzazi alifariki dunia saa chache baada ya kujifungua.
“Wao kama Wakurya waliamini kwamba mama yake aliona chatu wakati akiwa mjamzito ndiyo maana mtoto akazaliwa hivyo.
“Chacha kwa sasa anasoma kidato cha kwanza kwa shida. Wanafunzi wenzake wanamnyanyapaa na kumuoneshea vidole kila anapopita,” alisema mtu huyo ambaye ndiye mwangalizi wa karibu wa maisha ya Chacha.
“Kwa sasa, Chacha anaishi na baba yake na babu yake na hali yao kiuchumi si nzuri na ndiyo maana tumewaomba nyie Global mtusaidie.”
No comments:
Post a Comment