airport jogging

mavazi

aus521

aus9

Showing posts with label BONGO MOVIE. Show all posts
Showing posts with label BONGO MOVIE. Show all posts

Tuesday, January 16, 2018

MABINTI WA CHIBOK WALIOTEKWA NA BOKO HARAM WAGOMA KURUDI NYUMBANI

Kundi la Boko Haram limetoa video mpya ikionyesha wasichana 14 waliotekwa katika mji wa Chibok, Kaskazini mwa Nigeria mnamo mwezi Aprili 2014 ambapo katika video hiyo wamesema kamwe hawatarejea nyumbani kwa sababu sehemu wanayoishi sasa ni takatifu na wanapata kila wanachohitaji.

Mabinti 300 wa Shule ya Chibok walitekwa na kundi la kigaidi la Boko Haram mwaka 2014 ambapo baadhi yao walifanikiwa kutoroka licha ya wenzao kubaki na hawajulikani walipo. Kumekuwa na picha na video ambazo Boko Haram huzitoa mara chache ili kuwaumiza wazazi wao.
Kundi hilo limekuwa maarufu katika ukanda wa Afrika Magharibi kufanya vitendo vya kihalifu ikiwemo mauaji ya kinyama miongoni mwa raia. Inasemekana mabinti hao wanawatumikisha kingono.

Muigizaji wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’. Muigizaji wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amepata pigo kwa kuondokewa na mama yake mzazi. Mungu ailaze roho ya mama Johari mahala pema peponi, Amina.

Muigizaji wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
Muigizaji wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amepata pigo kwa kuondokewa na mama yake mzazi. Mungu ailaze roho ya mama Johari mahala pema peponi, Amina.

Sabrina Rupia ‘Cathy’. MKONGWE wa sinema za Kibongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ ameamua kutupa sanaa kule kisha kujiweka pembeni kwa kile alichosema kwamba, hailipi na amejikita zaidi kwenye kuuza chakula. Cathy aliiambia Za Motomoto News kuwa, kwa sasa amejikita kwenye kupika vyakula ambavyo anasambaza sehemu mbalimbali anapopata oda na imekuwa ikimlipa tofauti na filamu hivyo ameiweka sanaa pembeni kwanza maana kazi ya kupika haina umri na wala haimtupi mtu. “Kupika na kuuza chakula sasa hivi ndiyo habari ya mjini, kwa sasa akili na nguvu zangu zote nimezielekeza kwenye kazi hii ya kupika maana maisha ni magumu sana nikitegemea sanaa tu na nina watoto nitafeli,” alisema Cathy.

Sabrina Rupia ‘Cathy’.
MKONGWE wa sinema za Kibongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ ameamua kutupa sanaa kule kisha kujiweka pembeni kwa kile alichosema kwamba, hailipi na amejikita zaidi kwenye kuuza chakula.

Cathy aliiambia Za Motomoto News kuwa, kwa sasa amejikita kwenye kupika vyakula ambavyo anasambaza sehemu mbalimbali anapopata oda na imekuwa ikimlipa tofauti na filamu hivyo ameiweka sanaa pembeni kwanza maana kazi ya kupika haina umri na wala haimtupi mtu.

“Kupika na kuuza chakula sasa hivi ndiyo habari ya mjini, kwa sasa akili na nguvu zangu zote nimezielekeza kwenye kazi hii ya kupika maana maisha ni magumu sana nikitegemea sanaa tu na nina watoto nitafeli,” alisema Cathy.

Tuesday, October 31, 2017

Joti kawajibu wanaomsema kwa kunyoa kiduku kwenye harusi yake



Jumamosi iliyopita ilikua harusi ya Mchekeshaji maarufu Tanzania Lucas Muhavile maarufu kama Joti ambapo gumzo lilikua pia nywele zake alizonyoa kwa staili ya kiduku na kuingia nacho Kanisani jambo ambalo lilifanya baadhi ya watu kuongea sana kwenye mitandao.
Jana AyoTV na millardayo.com zinae Joti kwenye Exclusive Interview ambapo amewajibu waliomsema kuhusu kiduku chake, >>> “Sidhani kama kuna sheria au kuna maandiko yameandika kwamba ukinyoa hivi hutakiwi kufunga ndoa, hii sanasana iko kwenye maadili tu
“Nilimuomba Padri na akanielewa na kuniambia wewe ni Msanii tunajua cha kufanya usisuke tu, fumua hizo nywele ziwe tu kawaida zibanebane vizuri”

Tuesday, January 3, 2017

BEN SELENGO anaendelea vizuri baada ya kupata ajari mbaya.......

Msanii wa filamu Ben Selengo baada ya kupata ajali ambaya siku ya sikukuu ya Christmas na kulazwa katika Muhimbili, ameruhusiwa na sasa hivi yupo nyumbani.

Mchekeshaji huyo amedai licha ya kuwa ameruhusiwa kutoka hospital lakini bado afya yake haijakaa sawa na anahitaji maombi.
“Bado nahitaji maombi yenu wadau,” aliandika Ben Instagram “nimetoka Muhimbili nipo home ila kiafya bado,”

Hili ni gari ambalo alipata nayo ajali

Thursday, October 15, 2015

MR. CHUZ AACHANA NA FILAMU

Mkongwe kwenye gemu la filamu Bongo, Tuesday Kihangala ‘Mr. Chuz’.
Gladness Mallya
MKONGWE kwenye gemu la filamu Bongo, Tuesday Kihangala ‘Mr. Chuz’ ameamua kuachana na filamu kwa kile alichodai kwamba hazilipi.

ROSE NDAUKA: SITAKI KUWACHANGANYA MASHABIKI

 
Gladness Mallya
MWANADADA staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka amesema hataki kujihusisha na harakati za siasa kwa sasa kwa vile anaogopa kuwachanganya mashabiki wake.
Mwanadada staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
Akipiga stori na gazeti hili, Rose alisema kwa kuwa yeye ni kioo cha jamii anayeelimisha kupitia kazi yake, alisema kujiweka wazi upande ulipo ni kuwagawa watu wake

MAJUTO AREJEA TOKA MAKKA SHAVU DODO!

Gladness Mallya na Hamida Hassan
MABADILIKO! Baada ya kunusurika kwenye vifo vya mkanyagano vilivyoua mahujaji zaidi ya 4000 waliokwenda kuhiji katika mji wa Mina, Makka nchini Saudi Arabia, staa wa filamu za Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ amerejea salama akiwa shavu dodo na kusema ameachana na maisha ya zamani, sasa amekuwa mtu wa tofauti kabisa.

Staa wa filamu za Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ alipowasili toka kuhiji Makka.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko katika mahojiano maalum mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jumamosi iliyopita na kupokewa kifalme, kwani mamia ya ndugu waliofika uwanjani hapo kuwapokea mahujaji wengine, walitaka kumpa mkono na kupiga picha na staa huyo wa vichekesho nchini .
SANAA BASI?
Alisema: “Nimerudi salama jamani. Lakini nimejifunza mengi sana kule Makka. Tamko langu kubwa kuhusu sanaa ni kwamba, sitacheza tena filamu zinazohusu mapenzimapenzi wala kushiriki matangazo ya kwenye runinga yenye mwelekeo wa mapenzi. Sitaingia tena baa. Pia masuala ya wasichana ‘dogodogo’ ambao wamezoea kunishobokea wanatakiwa wapite mbali na mimi.
“Lakini pia kuna hii tabia ya wasichana kutaka kupiga picha na mimi kwa kutumia simu za Smart Phone, wenyewe mnaita ‘selfie’ sitaki kwani mambo yote hayo ni chukizo kwa Mwenyezi Mungu na yatanirudisha nilikokuwa zamani, sitaki nitoke kwenye maisha yangu ya sasa yaliyobaki hapa duniani.”

....Akipokelewa na ndugu zake.
AWEKA KIAPO
Mzee Majuto alikwenda mbele zaidi kwa kusema kwa sasa ataishi maisha ya kitakatifu zaidi, ambapo kwa mwezi atatumia siku kumi kusafiri sehemu mbalimbali za nchi kwa ajili ya kuwafundisha watu mafundisho ya Mwenyezi Mungu.
“Ukweli sasa nimekuwa mtu wa ibada kila mara. Kama ni filamu nitacheza zile ambazo hazimchukizi Mwenyezi Mungu. Na muda mwingi nitawafundisha watu mafundisho ya Mwenyezi Mungu. Nikiona sanaa inaniingiza majaribuni nitaachana nayo kabisa kwani tayari nimeshajenga msikiti na madrasa kule Tanga,” alisema Mzee Majuto.
AOMBA AOMBEWE
Alisema: “Mimi ni binadamu, hivyo kwa nguvu zangu na akili zangu sitaweza kuyatimiza hayo, hivyo nawaomba Watanzania waniombee ili niishi maisha ya kumpendeza Mwenyezi Mungu na nisirudi kule nilikokuwa zamani.”
ALIVYONUSURIKA KUFA MAKKA
Aidha, Mzee Majuto alianika jinsi yeye na mahujaji wengine walivyofanikiwa kumaliza ibada ya hija salama Makka na mahujaji wote wakaelekea kwenye kutimiza nguzo tano za Kiislamu za kumpiga mawe shetani Mina ambako huko ndiko maafa ya kukanyagana yalitokea.
Alisema: “Nilikuwa tayari kwenda

RAYUU: WANAUME WANNE WAMEINGIA MITINI

Msanii wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’.

MAYASA MARIWATA
NYOTA wa filamu Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amesema anajihisi kama mwanamke mwenye mkosi baada ya wanaume wanne alioshiriki nao mapenzi kuonesha nia ya kumuoa, lakini ghafla waliingia mitini na kupeperusha ndoto yake ya kuwa mke wa mtu.

KAMPENI ZAMBADILISHA AKILI JOHARI

Sta wa sinema za kibongo, Blandina Chagula maarufu kama Johari.
aus9
BLANDINA Chagula maarufu kama Johari, ambaye ni mmoja wa wasanii wanaozunguka nchi nzima kuipigia kampeni CCM katika uchaguzi mkuu, amesema baada ya kutembea na kufanya kazi, amejikuta akiihamishia akili yake katika siasa.

Monday, June 8, 2015

JOKATE AMLIPUA DIAMOND!

aus9
Jino kwa jino! Sexy lady anayefanya poa na ngoma yake ya Leo Leo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, amemlipua aliyewahi kuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye hivi karibuni alimwita makombo baada ya kusikia kwa sasa anatoka kimalovee na msanii Ali Kiba.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
Akizungumza na gazeti namba moja la mastaa Bongo, Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Jokate alisema alishangazwa na maneno hayo ambayo hakustahili kuyatamka kwani kama ni ishu ya mtu kula makombo mbona hata yeye ni makombo na bado anakula makombo?
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’
“Sijapendezwa na kauli ya Diamond na namshangaa sana, sijajua nini kimemkuta maana mimi sijamtaka wala hakuna ambapo niliwahi kumwambia kuwa ninatoka  au ninamtaka Kiba, zaidi ya maneno ya watu kwenye mitandao ya kijamii.
“Hata kama hilo lipo, bado sioni maana ya neno makombo kwani hata yeye ni makombo na anakula makombo kwa Zari (Zarinah Hassan) kwani nani asiyejua?” alihoji Jokate akionekana kuchukizwa na kauli hiyo ya Diamond na kuongeza:
“Yawezekana labda maana ya neno hilo hatulijui ndiyo maana tunalisema bila kuliangalia kwa umbali zaidi, hivyo ninachoweza kukisema ni kwamba mimi sijawahi kumtaka wala kumhitaji hivyo sioni kabisa sababu ya msingi ya kusema hivyo labda kama alikuwa na maana nyingine tofauti na hiyo.”

Wednesday, June 3, 2015

IRENE PAUL, DAVINA NUSU WACHAPANE!

na aus9
UBABE? WASANII katika tasnia ya filamu, Irene Paul ‘Smart Girl’ na Halima Yahaya ‘Davina’ wamejikuta wakitaka kuzichapa kavukavu baada ya kushindwa kudhibiti hasira walipokuwa wakitaniana.
Irene Paul
Ishu hiyo ilitokea juzikati ndani ya Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar, kulipokuwa na mkusanyiko wa wasanii mbalimbali ndipo wawili hao walipotunishiana misuli.
Halima Yahaya ‘Davina’
Ishu hiyo iliibuka baada ya Davina kumtupia maneno ya kejeli mwenzake huku Irene akionekana kuwa ‘siriaz’ akitahadharisha kuwa hapendi utani na kuanza kumtupia maneno makali jambo lililowafanya baadhi ya wasanii kutuliza hali ya hewa.
Mwandishi wetu aliyeshuhudia tukio hilo mita chache na mahali alipokuwa, alishuhudia Davina naye akimpa maneno makali mwenzake ndipo wakataka kuzichapa lakini bahati nzuri wakaamuliwa

Thursday, April 23, 2015

HIVI WASANII MTAKUWA NA UCHUMBA‭, ‬NDOA ZA MAIGIZO MPAKA LINI‭?‬

Kwenu mastaa wa tasnia mbalimbali Bongo‭, ‬habari zenu bwana‭. ‬Poleni na majukumu ya kila siku ya kulijenga taifa‭.‬
Mkitaka kujua afya yangu‭, ‬mimi ni mzima‭, ‬namshukuru Mungu naendelea kutimiza majukumu yangu‭, ‬likiwemo hili la kuwaandikia barua‭.‬
Nimewakumbuka leo kupitia barua‭, ‬nataka kuwaambia kwamba mimi pamoja na mashabiki wengine wa sanaa yenu tumewachoka‭. ‬Tumechoka kuona na kusikia kila siku mkifanya maigizo kwenye maisha yenu halisi‭.‬
Hivi ni kwa nini kila kukicha tunasikia mnaachana‭? ‬Kwa nini hamdumu kwenye uhusiano wa mapenzi‭? ‬Kwa nini hamdumu kwenye ndoa kama mashabiki wenu wanavyowategemea‭?‬
Penzi linapoanza kushamiri‭, ‬mnalinadi kwenye mitandao na vyombo vya habari‭. ‬Mnawaaminisha mashabiki wenu kuwa mnapendana kwa kauli zenu motomoto lakini ndani ya miezi miwili mitatu penzi chali‭.‬Wengine mnaonesha kwamba mmedhamiria na kuamua kufunga ndoa kabisa‭, ‬lakini kumbe moyoni bado mnakuwa mna lenu jambo‭. ‬Mashabiki wenu wanafurahia kuona mmeoana lakini ndoa nayo haidumu‭, ‬mnaachana‭.‬
Mbaya zaidi mnapoachana mnapeana maneno ya kashfa‭, ‬mnaumbuana kiasi ambacho kinadhihirisha kabisa mlikuwa hamna mapenzi ya dhati‭ ‬au hamkudhamiria kabisa kuingia kwenye ndoa‭.‬Hivi kama kweli mlipendana‭, ‬nini kinawafanya muanze kuumbuana‭? ‬Badilikeni‭, ‬mashabiki wenu wamechoka kusikia kila kukicha ndoa ya‭ ‬staa fulani imevunjika‭, ‬wachumba fulani wameachana‭, ‬ni aibu‭.‬
Watu hawapendi kuona Nay wa Mitego na Siwema mkiwa mmeachana‭. ‬Tena mnaachana kwa kupeana maneno yanayoonesha kwamba mlikuwa hamna nia ya dhati ya kuwa wapenzi‭.‬Shamsa Ford na Dick‭, ‬kapo yenu ilikuwa nzuri‭. ‬Mlipamba vyombo vya habari‭, ‬uhusiano wenu ukazaa matunda ya mtoto mmoja lakini ndoto ya kuishi kama mume na mke imeyeyuka‭.‬
Nasibu Abdul‭ ‬‮!‬٪Diamond‮!&‬‭ ‬na Wema Sepetu penzi lenu lilikuwa likipendwa‭  ‬na wengi‭, ‬likaishia njiani‭. ‬Rose Ndauka na Malick Bandawe mlioishi na kubahatika kupata mtoto mmoja‭, ‬nini kiliwakuta‭? ‬Inasikitisha‭.‬Wolper na Dallas nao walipamba sana vyombo vya habari lakini mwisho wa siku chali‭. ‬Ndugu zangu‭, ‬mnapaswa kubadilika‭. ‬Msiigize maisha yenu‭. ‬Igizeni kwenye filamu‭, ‬mkirudi nyumbani mjitambue kwamba heshima‭, ‬upendo‭, ‬busara vinahitajika ili kuishi na mwenzako‭.‬
Mbona wapo wasanii wengi tu maarufu duniani na wamedumu kwenye uhusiano‭? ‬Kwa nini msiige mfano kwa mastaa kama Marlaw na mkewe‭, ‬Jay Z na Beyonce ambao wanaheshimu penzi lao hadi sasa‭?‬Jamani‭, ‬cha msingi mnapaswa kuheshimu suala la uhusiano‭, ‬msifanye masihara katika maisha ya ukweli‭.  ‬Vitu vingine vinapaswa kufanyika kwenye filamu pekee na siyo kuvihamishia katika maisha halisi‭.‬
Bila shaka mtakuwa mmenielewa na mtabadilika‭, ‬kila la kheri‭.

Wednesday, April 15, 2015

NIKITA; MSANII WA KIKE ANAYECHEZA FILAMU ZA MAPIGANO BONGO

aus9

GWAJIMA AWAACHA WAUMINI WAKE NJIA PANDA

aus9
MCHUNGAJI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amewaacha waumini wake njia panda kufuatia kauli yake ya kuwataka wamsindikize Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati jijini Dar, jana alipokwenda kuhojiwa huku Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akiwa ametoa tamko la kuzuia waumini hao kukusanyika kituoni hapo.
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
Gwajima aliyetoa kauli hiyo kwa waumini wake katika ibada ya Jumapili iliyopita kanisani kwake, Kawe jijini Dar, alitarajiwa kufika kituoni hapo kujibu tuhuma za kumtusi Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinari Pengo.
Wakizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutoandikwa majina yao, juzi jijini Dar, baadhi ya waumini wa Gwajima walisema wanashindwa kufanya uamuzi wa kumsindikiza kiongozi huyo kwani jeshi la polisi limesema halitaruhusu mtu kumsindikiza.
“Kusema kweli tumebaki njia panda maana mchungaji amesema twende tumsindikize lakini Kova naye kasema jeshi la polisi litatumia nguvu kuwatawanya watu ambao watakaidi amri hiyo ya jeshi la polisi,” alisema muumini mmoja huku waumini wenzake wakiunga mkono.
Wakati Gwajima alipowataka waumini wake wamsindikize kituoni hapo, Kova alisisitiza kuwa kiongozi huyo wa dini anatakiwa kufika kituoni hapo akiwa na mwanasheria wake pamoja na watu wachache tu wa karibu hivyo kuwafanya waumini wengi wa kanisa la Gwajima kubaki njia panda.
Kupitia video inayomuonesha Gwajima akimtupia maneno makali Pengo, mchungaji huyo wa Ufufuo na Uzima alimtuhumu Pengo kuwa amewasaliti maaskofu wenzake waliotoa tamko la kuipigia kura ya ‘Hapana’ Katiba Inayopendekezwa kwa kile walichodai haikukidhi matakwa ya wananchi

Tuesday, March 24, 2015

JINI KABULA AFAKAMIA ‘MIKUKU’ UWANJANI!

Uroho? Mwigizaji wa sinema za Kibongo aliyeibuliwa na mchezo wa runingani wa Jumba la Dhahabu, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ juzikati alinaswa akifakamia minofu ya kuku katika ya kadamnasi iliyojitokeza katika Dimba la Taifa jijini Dar.

Wednesday, March 18, 2015

AIBU ILIYOJE: MKE AVAA KININJA, AMFUATILIA MUMEWE, AMFUMANIA

WAANDISHI WETU, MWANZA
Aibu iliyoje! Tukio la aina yake limetokea maeneo ya Diluxe jijini hapa baada ya mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Faudhia almaarufu mama Baraka kumfumania mumewe akisaliti ndoa yao mbichi.
Faudhia akihamaki baada ya kufumaniwa.
Kwa mujibu wa mama Baraka, amekuwa akimfuatilia mumewe kwa muda mrefu baada ya kutonywa na wambeya kuwa baba mtoto wake huyo amekuwa akichepuka na ‘kichenchede’ (mrembo) wa mjini.
Siku ya tukio, hivi karibuni ilidaiwa kwamba mume huyo alirudi nyumbani mapema, akapumzika kidogo, majira ya saa sita mchana aliamka, akaoga na kupewa chakula kama kawaida kisha akamuaga mkewe kuwa anaenda ofisini kuna dharura imetokea ghafla.
...Akiwa anavaa.
Kwa mujibu wa mke huyo, jamaa alipotoka tu naye akachukua pikipiki ambayo ilikuwa tayari imeandaliwa na kuanza kumfuatilia kwa nyuma kila alipokuwa anaenda ambapo alienda katika baa mbalimbali za Villa Park Resort, Kibo na nyingine.
Ilisemekana kwamba, alipofika Diluxe Night Club, alipiga honi kisha akajitokeza kimwana mmoja na kuingia kwenye gari hilo wakaondoka, walipofika kwenye eneo la giza maeneo hayohayo ya Diluxe Night Club, gari lilisimama, wakashuka, wakahamia siti ya nyuma.
OFM WAPIGIWA SIMU
Kamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers na vijana wake, wakiwa katika pikipiki zao ziendazo kasi wakisakanya habari maeneo ya Jiji la Mwanza ghafla walipokea taarifa kutoka kwa chanzo chao kuwa kuna tukio maeneo hayo.
OFM walifika maeneo hayo na kukuta timbwili la nguvu ndani ya gari huku mama mmoja aliyevaa kininja akimwadhibu msichana aliyekuwa nusu utupu na mumewe ndani ya gari.Wakati wa timbwili hilo, mchepuko alivaa suruali na kusahau kuvaa kufuli pakaendelea kuchimbika.
MAMA BARAKA AFUNGUKA
Akizungumza na OFM akiwa eneo la tukio, mama Baraka alisema kuwa alikuwa na kazi kubwa ya kumfuatilia mumewe kwa siku nyingi lakini mumewe huyo alikuwa akipiga chenga.“Nilianza kumfuatilia mume wangu kwa muda mrefu sana baada ya kupata taarifa kuwa huwa ana tabia ya kufanya mapenzi kwenye gari na wanawake.“Nilishamuuliza zaidi ya mara tatu kutaka kujua kama kweli ana tabia hiyo lakini alinikatalia katakata.”

MUME ATAKA KUKATA MSHIKO
Mume huyo alipoulizwa juu ya tabia hiyo alikataa katakata kuongea na kuwambia makamanda wa OFM kuwa hayo mambo anaomba yaishie hapohapo kisha kuzama kwenye waleti na kutoa fedha.
Hata hivyo, makamanda wetu walizikataa na kuendelea kufanya kazi yao kwa mujibu wa kiapo chao cha kutopokea hongo wala rushwa hivyo waliondoka eneo hilo wakimwacha mama Baraka akipambana na mumewe huku binti akiachiwa aende zake

BABA: ROSE NDAUKA OLEWA SASA!

CHANDE ABDALLAH/Amani
BABA mzazi wa staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka, Donatus Ndauka anadaiwa kumtaka mwanaye huyo kuangalia uwezekano wa kuingia maisha ya ndoa kwa vile siku zinakatika kama mvua za masika.
Staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka.
Kwa mujibu wa chanzo, baba huyo mwenye makazi yake jijini Tanga alimpigia simu mwanaye mapema wiki hii baada ya kusoma habari kupitia Magazeti ya Global ikimkariri mzazi mwenzake na staa huyo, Malick Bandawe akisema hakuna mwanamke kama Rose.
Malick alisema licha ya kumwagana na Rose mwaka jana, lakini bado anamkumbuka na kumthamini kama mzazi mwenzake kwa vile ndiye anabeba jukumu la kumwangalia mtoto wao, katika maisha ya kila siku.
“Baba yake alimwambia Rose kama kuna mwanaume anayesema anampenda kwa sasa basi amuoe na si kupoteza muda kwani siku zinakwenda sana. “Pia baba yake alimwambia anajua aliachana na Malick lakini kama ataona kuna mawazo yanamshauri kujenga upya uhusiano wao uliobakiza ndoa tu, aangalie mwenyewe Rose kwa vile ni mtu mzima sasa, ila asichopenda baba yake ni kusikia leo huku, kesho kule,” kilisema chanzo hicho.
Amani lilimtafuta Rose kwa njia ya simu ambapo lilipomuuliza kama kweli alipewa ujumbe huo na baba yake alisema: “Iwe kweli au si kweli, kuna mambo ya familia, pia kuna mambo ya jumuiya.
Sasa kama kweli niliambiwa hivyo na baba yangu unataka na wewe nikwambie ili iweje?”
Amani: “Wewe ni staa bwana, lolote kwetu ni habari.”
Rose: (akakata simu).

SMS ZA MAPENZI ZA KAJALA NA BWANA ALIYEKUWA WA WEMA ZANASWA

DEOGRATIUS MONGELA/Amani
BAADA ya taarifa za mwigizaji Kajala Masanja kudaiwa kumuibia bwana aliyekuwa shosti yake, Wema Sepetu kudumu kwa muda mrefu na kukosa ushahidi wa moja kwa moja, hatimaye ushahidi wa SMS za mapenzi za Kajala na bwana huyo wa Wema ambaye ni kigogo zimenaswa, Amani linakumegea mchongo kamili.
Staa wa Bongo Movie, Kajala Masanja.
Chanzo makini kilichokuwa karibu na Kajala na kigogo huyo, kilipenyeza habari kuwa kimefanikiwa kuzinasa meseji za Kajala kupitia kwenye simu ya kigogo huyo ambaye alidumu katika penzi na Wema kisha kumwagana baada ya Kajala kuingilia kati.
“Nimetumia ujanja wa hali ya juu hadi nikafanikiwa kupata SMS za Kajala na yule kigogo wa Wema, kama vipi niwatumie,” kilisema chanzo chetu.Kama hiyo haitoshi, chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, SMS hizo zilionesha namna Kajala alivyokuwa akiitana baby na kigogo huyo, huku wakiwa ‘dip kimalovee’ kiasi cha kigogo huyo kuwagharamia wazazi wa Kajala mahitaji mbalimbali.
Staa wa Bongo Movie, Wema Spetu.
“Jamaa walikuwa wanapika na kupakua, kigogo alikuwa akigharamia kila kitu, kuanzia misosi ya nyumbani, usafiri wa location na hata kwa wazazi wa Kajala, alikuwa anatuma fedha,” kilisema chanzo hicho.
Mwanahabari wetu alifanikiwa kuzinasa SMS hizo na kujionea zikiwa na majibizano ya muda mrefu huku zikitaja pia marafiki wa Kajala anaofanya nao kazi kwa muda mrefu.
Baada ya paparazi wetu kumwagiwa SMS hizo, alimvutia waya Kajala ambaye alizikana SMS hizo na kuomba atumiwe ndipo atoe jibu ambapo mwandishi wetu alifanya hivyo lakini hakujibu chochote na hata alipopigiwa tena, hakupokea.