airport jogging

mavazi

aus521

aus9

Showing posts with label serikali. Show all posts
Showing posts with label serikali. Show all posts

Tuesday, January 16, 2018

MAMBOSASA: BAADHI YA WAFUNGWA WALIOACHIWA NA JPM WANAFUKUA SILAHA ZAO

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limedai kuwa linazo taarifa kwamba baadhi ya wahalifu walioachiwa kwa msamaha wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli wameanza kufukua silaha zao walizokuwa wamezificha ili zifanye kazi ya uhalifu katika maeneo mbalimbali huku akisema hawatasita kuwarudisha tena jela iwapo wataendelea na tabia za uhalifu.

Tuesday, October 31, 2017

“Hawapumui na wakipumua wanapumulia gerezani” – Rais Magufuli.





Hii kauli inatoka kwenye siku ya kwanza ya ziara ya siku mbili ya Rais Magufuli Mwanza, amehutubia Wananchi kwenye viwanja vya Mwatex Nyakato na moja ya nukuu za kauli zake ni hii ya “siku hizi hawapumui na wakipumua wanapumulia gerezani” tazama hii video hapa chini kupata yote mengine aliyoyasema Mr. President

BREAKING NEWS

Habari zilizotufikia muda huu ni kwamba Mbunge wa Kigoma Mjini ambae pia ni kiongozi wa chama cha ACT WAZALENDO Zitto Kabwe amekamatwa na polisi.



Taarifa zaidi zinasema Zitto amekamatwa akiwa nyumbani kwake Dar es salaam na kupelekwa kituo cha Polisi Chang’ombe, habari hii imethibitishwa na Afisa Habari wa ACT Wazalendo Abdallah Khamis ambaye ameeleza kuwa sababu za kukamatwa kwake ni hotuba aliyoitoa juzi katika kata ya Kijichi.

Wednesday, January 4, 2017

HIKI ndicho kilichovunja ndoa ya Mkwasa na TFF



TFF limesema, kuachana na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Charles Boniface Mkwassa “Master” ni makubaliano ya kimkataba kwa pande zote mbili na hakukuwa na tofauti zozote ziliyojitokeza.

Afisa habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfred Lucas amesema, wanatarajia kumalizana kabisa na Mkwasa mpaka ifikapo mwezi wa Machi mwaka huu ikiwemo fidia za kukatisha mkataba.

MTU mmoja amenusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa risasi na askari wa wanyamapori Sumbawanga


Mtu mmoja amenusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa risasi na kujeruhiwa mguu wa kulia na askari wa wanyamapori wa pori la Akiba la Uwanda kwa madai kuwa alikatisha kwenye hifadhi kinyume cha sheria.

Tuesday, September 15, 2015

MAFUFU ASHUSHIWA KIPIGO NA MKEWE!

KIPIGO! Licha ya kujulikana na kuogopeka kwa ukorofi na ubabe uliopitiliza, muigizaji wa filamu za Kibongo, Jimmy Mafufu, amechezea kichapo kutoka kwa mkewe wa ndoa, Salma Mafufu kwa kile kilichoelezwa kuchelewa kurudi nyumbani

Wednesday, September 2, 2015

Rais Kikwete aagwa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama



Askari wa Vikosi mbali mbali vya Ulinzi wakiwa katika uwanja wa Taifa wa Uhuru Jijini Dar es Salaam  katika sherehe za kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete alipoagwa rasmi na Vikosi hivyo leo,[Picha na Ikulu.]
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi la Vikosi vya  Ulinzi wakiwa katika uwanja wa Taifa wa Uhuru Jijini Dar es Salaam  kumuaga kwa kumaliza muda wake wa Urais leo.[Picha na Ikulu.]
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipowasili katika uwanja wa Taifa wa Uhuru Jijini Dar es Salaam  katika sherehe za kuagwa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama leo,[Picha na Ikulu.]

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete (wan ne kushoto) akiwa na Viongozi wengine wakisimama kupokea salamu ya heshma ya kwaride la Vikosi vya Ulinzi wakati wimbo wa Taifa ulipopigwa katika uwanja wa Taifa wa Uhuru Jijini Dar es Salaam  katika sherehe za kuagwa rasmi leo,[Picha na Ikulu.]