airport jogging

mavazi

aus521

aus9

Showing posts with label udaku. Show all posts
Showing posts with label udaku. Show all posts

Wednesday, January 4, 2017

RAPPER Feature auanza mwaka mpya kwa style ya Wema Sepetu



Rapper wa Marekani, Future ameamua kuuanza mwaka mpya wa 2017 kwa kufuta picha zote kwenye mtandao wa Instagram.

Akaunti ya rapper huyo ina followers wapatao milioni 8.7 huku akiwa amemfollow mtu mmoja pekee ambaye ni Dj Esco.


Future anaungana na malkia wa filamu Bongo, Wema Sepetu ambaye na yeye aliamua kuuanza mwaka kwa kitendo kama hicho cha kufuta picha zake kwenye mtandao huo

40 Ya Mdogo Wa Tiffah Usipime, Mastaa Wakubwa Afrika Watajwa Kuhudhuria


STORI: GABRIEL NG’OSHA, GAZETI LA UWAZI, TOLEO 1021, JANUARI 3-9, 2017

DAR ES SALAAM: Habari ya motomoto inaeleza kuwa Januari 16, mwaka huu ndiyo siku ambayo mtoto wa kiume wa staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Nillan Nasibu ‘Chibu Junior’ atatimiza siku 40 tangu alipozaliwa Desemba 6, mwaka jana.

NAY ataja tofauti ya Diamond na Alikiba


Rapa Nay wa Mitego amefunguka na kuweka wazi kuwa katika wanamuziki watatu wakubwa Tanzania wazuri kwake yeye Alikiba atakuwa namba moja ila katika wanamuziki wakubwa watatu wafanyabiashara basi Diamond Platnumz atakuwa namba moja.Nay ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Sijiwezi', amesema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo cha EATV na kusema siku zote yeye amekuwa akimkubali sana Alikiba ingawa anatambua wazi mtaani kuna tetesi kuwa hawezi kufanya naye kazi kutokana na yeye kuwa na uswahiba

POLISI kufukua kaburi la binti aliyezikwa kwa siri Arusha


Familia moja  jijini Arusha inadaiwa kumzika kwa siri mtoto wao mdogo wa kike wa miaka mitatu katika kaburi lililofichwa, huku majirani wakidanganywa kuwa binti huyo yupo hai.

Tuesday, January 3, 2017

Mkulima aliyechomwa mkuki arejea nyumbani

Wiki iliyopita kulikuwa na habari iliyowashtua watu kwa namna moja au nyingine. Ni habari ya mkulima na mkazi wa kitongoji cha Upangwani, kijiji cha Dodoma Isanga, Kata ya Masanze, Kilosa mkoani Morogoro ,Augustino Mtitu(35), aliyechomwa mkuki mdomoni. Hatimaye kijana huyo ameruhusiwa kutoka hospitali alikokuwa amelazwa na kurejea nyumbani.

Madaktari wamesema kuruhusiwa kwa mgonjwa huyo kumetokana na yeye kupona kufuatia kufanyiwa

Karrueche awagombanisha Chris Brown na Soulja Boy

Mwaka 2017 umeanza vibaya kwa Chris Brown na Soulja Boy – kwakuwa wameanzisha bifu chanzo kikiwa ni mrembo Karrueche Tran.

Tangu alipoachana na Karrueche Chris amekuwa akimfuatilia mrembo huyo huku mara kadhaa akigombana na wanaume ambao wanaomtolea udenda. Na sasa balaa limemkumba rapper Soulja Boy baada ya kulike picha ya mrembo huyo kwenye mtandao wa Instagram kitendo ambacho kimeonekana kumkera Brown.
Soulja Boy amefunguka kupitia mtandao wa Twitter kuwa Chris amemtafuta na kumpiga mikwara baada ya kulike picha hiyo

Tuesday, June 7, 2016

Chuchu Hans adaiwa kunasa ujauzito


Chuchu-HansChuchu Hans.
IMELDA MTEMA
STAA wa filamu Bongo, Chuchu Hans anadaiwa kunasa ujauzito wa mchumba wake ambaye naye ni staa wa filamu, Vincent Kigosi ‘Ray’. Kwa mujibu wa chanzo ambacho kipo karibu na wawili hao, Chuchu kwa sasa ni mtu wa kujifungia ndani na amekuwa hapatikani kwenye matukio mbalimbali yanayomhusu. “Ameshanasa, tena ujauzito huo ni wa Ray, unaambiwa sasa hivi kawa mtu wa kujifungia ndani tu na kitumbo kimeshamtoka,” kilisema chanzo.
CHUCHU789111           Chuchu na Ray
Alipotafutwa Chuchu kujua ukweli alijibu; “Nashangaa, watu wengi wananifikiria hivyo lakini sitaki kuongea chochote. Labda watakuwa na husda tu ndiyo maana wananifikiria hivi,” alisema Chuchu. Ray alipotafutwa kwa njia ya simu ili kusikia kauli yake hakupokea

Esha ‘alia’ wivu kwa hausigeli wake


ESHA35GLADNESS MALLYA
S TAA wa filamu za Kibongo, Esha Buheti ‘amelia’ wivu kwa mfanyakazi wake wa ndani (hausigeli) kuwa katika maisha yake ya ndoa hapendi kumwachia ampikie mumewe kwani siyo maadili.
Akizungumza na Showbiz Xtra Esha alisema kuwa, hata mumewe akipikiwa na dada wa kazi huwa anajua kwani akikionja chakula tu lazima aulize mpishi ni nani kutokana kuwa na ladha ya tofauti. “Simwachii dada ampikie mume wangu, chakula chake napika mwenyewe labda niwe naumwa,” alisema Esha

Tukio la Ajabu Kaburini

kaburi

DAR ES SALAAM! Wakazi wa Mbagala Chalambe jijini Dar es Salaam, waliamka asubuhi na kukutana na tukio lililojaa maswali mengi huku majibu yakiwa haba kufuatia kukuta kitu kaburini kikiwa kimeviringishiwa sanda.
ILIVYOKUWA
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo lilijiri hivi karibuni kwenye Makaburi ya Chalambe ambapo wakazi hao walilizunguka kaburi hilo huku wakidai kuwa, ndani ya sanda hiyo kulikuwa na mtoto aliyeuawa na kuwekwa hapo.
SHUHUDA ATOA
MAWAZO YAKE
“Jamani humu kwenye sanda kuna maiti ya mtoto mdogo. Lazima kuna mahali ameuawa, wakamviringishia sanda maskini wa Mungu, wakaja kumuweka hapa,” alisema mkazi mmoja akiwa amejikunyata baada ya kutoka kulala.
IMG-20160522-WA0001MTAZAMO WA WENGINE
Wengine walisikika wakisema kuwa, kwa vyovyote mtu au watu waliotupa kitu hicho walikuwa katika harakati za ushirikina kutokana na maelekezo ya mganga.
“Huu ni ushirikina mkubwa, lazima watu wamefanya hivi kwa maelekezo ya mganga. Huwezi kuja kutupa vitu vya uchawi kwenye kaburi la mtu, watu hawana hata woga wala hawamuogopi Mungu,” alisema mama mmoja.

Tuesday, May 31, 2016

Prezzo amfuata Gigy Bongo!

Prezzo
IMEVUJA! Kumbe rapa mwenye jina kubwa Afrika Mashariki, Jackson Makini ‘Prezzo’moja ya ishu zilizomleta Bongo ni pamoja na kukutana na muuza nyago kwenye Video za Kibongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’.
Gigy Money
Akichonga na mtandao huu, Prezzo aliyewahi kubamba na Ngoma ya Nipe Nikupe akimshirikisha staa wa Bongo Fleva, Ambwene Yessaya ‘AY’ alisema kuwa, Gigy ni msichana ambaye amekuwa akimsikia siku za hivi karibuni Wakenya wakimzungumzia hasa juu ya vituko vyake jambo lililomfanya kuvutiwa kuonana naye.
“Gigy yuko hot mazee, nimemsikia sana Wakenya wakimzungumzia so nipo katika mpango wa kuonana naye, si unajua mimi nina mambo mengi, reality show na vitu vingine private,” alisema Prezzo. Gigy Money aliponyetishiwa ishu hiyo alifurahia jina lake kupaa hadi Kenya.

Baada ya Nay Kuchepuka… Lulu Diva Amgeukia Belle 9

lulu la diva (6)Lulu Diva
SIYO siri tena! Baada ya mkali wa Muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kuchepuka kwa msichana wa Kihabeshi mwenye asili ya Ethiopia, aliyekuwa mpenzi wake Lulu Abass ‘Lulu Diva’ naye ameamua kugeukia kwa staa wa muziki, Abedinego Damian ‘Belle 9’.
belle91Belle 9
Akizungumza na Over Ze Weekend Lulu ambaye ni muuza nyago kwenye video za Kibongo alidai kuwa, Nay hajatulia na badala yake anahitaji kuwa na mtu asiye na skendo za kutembea na wanawake ovyo na Belle 9 ndiye tulizo lake.
“Ni ukweli Nay nilikuwa naye kwenye uhusiano nikifahamu alishawahi kuwa na msururu wa wanawake lakini siyo siri yamenishinda na sasa nahitaji kujiweka kando. Sasa hivi feelings zangu zote zipo kwa Belle na analijua hilo,” alisema Lulu.

Kidoa Alamba Shavu la Kutangaza Nguo EBM

kidoa

STORI: HAMIDA HASSAN, WIKIENDA
VIDEO Queen Asha Salum ‘Kidoa’ hivi karibuni ameibua maswali mengi mtandaoni baada ya kutupia picha akiwa ameonesha nguo ya ndani ambapo wengi wamemkejeli kwa picha hizo.

Lungi alinanga penzi la Wolper, Harmonize

Harmonizer-na-Wolper 
Jacqueline Wolper na Rajab Abdulhan ‘Harmonize’
STORI: HAMIDA HASSAN, WIKIENDA
MSANII wa filamu wa kitambo, Lungi Maulanga amelinanga penzi na Jacqueline Wolper na Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ akisema kuwa, anachoona ni kama Wolper anatembea na mdogo wake.
LUNGI (1)Lungi Maulanga
Akiuzungumzia uhusiano wa mastaa hao, Lungi alisema alijisikia vibaya sana kuona shosti wake Wolper kafa, kaoza kwa Harmonize kutokana na tofauti kubwa iliyopo kati yao.
“Unajua Wolper ni kama mdogo wangu na shosti wangu hivyo siwezi kumuacha apotee, mimi nitamuita tutaongea kwa kina, kama atashikilia msimamo wake nitamuacha kwa sababu si unajua mtu akishapenda, lakini kiukweli hawajaendana,” alisema Lungi

Ishu Ya Kuchoropoa Mimba, Wema Kumfunga Jela Harmonize

WEMA2Wema Isaac Sepetu ‘Madam’
STORI: Mwandishi Wetu, Ijumaa
Dar es Salaam: Endapo mkali wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ atalivalia njuga suala la kudhalilishwa mtandaoni na msanii aliye chini ya Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Rajab Abdulhan ‘Harmonize’, jamaa huyo atakwenda jela miaka kadhaa na faini juu.
harmonize kasuku - bekaboyRajab Abdulhan ‘Harmonize’
CHANZO NI NINI?
Juzikati, Harmonize au Hamo, akiwa na kundi la wasanii wenzake katika eneo ambalo halikujulikana ni wapi, walijichukua clip (kipande cha video) kwa staili ya kujipiga ‘selfie’ huku Harmonize akiimba wimbo wa msanii Stamina uitwao Mwambie Mwenzio, ambao kwenye mistari hiyo dogo huyo alisherehesha kwa kusema kuwa, usitoe mimba usije ukaja kulia kama (Wema) Sepetu.
HARMONIZE ALA ZA USO
Baada ya Harmonize kuwaongoza vijana hao kumdhalilisha Wema kwa staili hiyo, watu wengi kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii walimpa jamaa huyo za uso, baadhi wakisema kuwa, umaarufu mdogo alioupata unamzuzua.
Wema SepetuWema na mama yake mzazi.
“Huyu mtoto anaona ameshakuwa maarufu sasa, anaona sawa kuwatukana hata wakubwa zake au ametumwa?” alihoji mmoja wa mashabiki wa Wema (Team Wema) aliyejitambulisha kwa jina la C_K kwenye Mtandao wa Instagram.
Mwingine akaandika: “Ninachojua huyu dogo anatafuta kiki lakini siyo kwa kufanya mambo haya, hivi ana ushahidi gani kama Wema katoa mimba?”
Harmonizer-na-Wolper 
Harmonize na Wolper
KAULI YA TCRA
Akizungumzia sakata hilo, Afisa kutoka Dawati la Malalamiko wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Doris Mhimbira alisema kuwa ni kosa la jinai ambalo mlalamikaji akiwa ‘serious’ anaweza kusababisha Harmonize akachukuliwa hatua kali za kisheria.

Tuesday, December 29, 2015

Davido na Tekno wanachangia penzi la Masogange?


Aggy31Agnes Masogange.
RIPOTI zimesambaa kwamba wanamuziki nyota wawili wa Nigeria, Davido na Tekno, huenda wanachangia penzi la mrembo wa Kitanzania, Agnes Masogange.
Mwezi Novemba mwaka huu mwimbaji Davido ambaye alivuma na album ya Omo Baba Olowo (Mtoto wa Tajiri) alijirusha na wasichana kadhaa wakati wa bethidei yake na mmoja wao alikuwa Masogane na baadaye zikaenea habari kwamba alikuwa mjamzito akitegemewa kumzalia Davido mtoto wa pili, lakini habari hizo baadaye zikakanushwa.
image (5)…..Akiwa na Tecno.
Kitu cha ajabu ni kwamba Masogange alianza kuweka na kufuta ujumbe mbalimbali kwenye mtandao ukionyesha alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Tekno kwa kula naye bata katika hoteli moja nchini Afrika Kusini.
Agnes-na-DavidoTekno naye alianza kutuma ujumbe kama huo, jambo lililowafanya mashabiki wake kuamini alikuwa na uhusiano na msichana huyo. Hata hivyo, mwimbaji huyo ameufuta ujumbe wote huo katika ukurasa wake

Monday, December 21, 2015

Mwanamke wa unga jela miaka 20


madawaAnna Gemanist Mboya.
Na Makongoro Oging’
Mrembo wa madawa ya kulevya ‘unga’, Anna Gemanist Mboya mkazi wa Kijitonyama, Kinondoni jijini Dar amefungwa jela miaka 20 na kupigwa faini ya shilingi milioni 148, fedha anazotakiwa kuzilipa mara atakapomaliza kifungo.
Mrembo huyo ambaye ni mfanyabiashara, amefungwa Desemba, Mosi, mwaka huu mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Wilfrida Koroso kwa kosa la kusafirisha madawa ya kulevya.
Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini, SACP Godfrey Nzowa (pichani) amethibitisha kuhukumiwa kwa mrembo huyo na ameipongeza mahakama kwa kasi ya kuendesha kesi nyingi za madawa ya kulevya na kuzitolea hukumu.
Kwa mujibu wa Kamanda Nzowa, Anna alikamatwa Januari 2, mwaka 2011 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kikosi kazi (task force) kilichopo katika kiwanja hicho.
awa“Nawaomba wananchi waendelee kuwafichua wahusika wa madawa ya kulevya ili waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria na kuokoa taifa letu na biashara hii haramu,” alisema Nzowa.
TUMIA LIKIZO HII KUJIANDAA VIZURI
NAFAHAMU kabisa kuwa

Monday, November 2, 2015

PETIT MAN, ESMA MAHABA UPYAA

Esma Abdul akiwa na aliyekuwa mumewe Hamad Manungwa ‘Petit man’.
Na Imelda Mtema 
Dada wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond,’ Esma Abdul amerudisha mahaba na aliyekuwa mumewe, Hamad Manungwa ‘Petit man’ baada ya kudaiwa kutengana, tena kwa talaka tatu.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, mpashaji wetu alisema Esma na Petit kwa sasa wako katika mapenzi motomoto na hivi karibuni walionekana pamoja wakiwa nyumbani kwa Wema Sepetu na mtoto wao, Taraj.
Gazeti hili lilimtafuta mwanaume huyo na kumuuliza juu ya ubuyu huo ambapo alisema; “Bado tuko kwenye maongezi, lakini sisi ni wazazi na hata juzi tulimpeleka mtoto kwa bibi yake ambaye ni Wema amuone, maana yule ni mtu muhimu sana kwangu,” alisema Petit man

DAVIDO AWAGOMBANISHA MASOGANGE, DIVA

Na Imelda Mtema

KITUKO! Mtangazaji wa kituo cha redio cha Clouds, Loveness Malinzi ‘Diva’ na Video Queen maarufu Bongo Agness Jerald ‘Masongange’ wamejikuta wakiingia katika ugomvi, kisa kikiwa ni msanii wa muziki wa Nigeria, Davido.

Video Queen maarufu Bongo Agness Jerald ‘Masongange’.
Akizungumza na gazeti hili, Masogange alimlaumu Diva, kwa kitendo chake cha kuandika katika ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram kuwa alizungumza na Davido ambaye alikana kuwa na uhusiano na msichana yeyote kutoka Tanzania.
Mtangazaji wa kituo cha redio cha Clouds, Loveness Malinzi ‘Diva’.
“Kinachonishangaza kwanini Diva afikie hatua ya kumpigia mpaka Davido kumuuliza kuhusu uhusiano wangu na mwanamuziki huyo, kitu ambacho kimeshangaza hata msanii mwenyewe,”alisema Masogange.
Masogange alionesha kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram meseji alizokuwa akimtumia mwanamuziki huyo, akishangazwa na dhamira ya swali hilo.“Inawezekana Diva anatafuta kiki kupitia jina langu, maana kila mtu anagombana naye, sasa huyo ni mtu wa aina gani jamani,” alisema Diva.
Diva, mmoja kati ya wanahabari wenye jina kubwa, alitafutwa kupitia simu yake ya kiganjani, lakini kwa muda mwingi iliita bila kupokelewa.

MADAI MAZITO; KAJALA AMHARIBU MWANAYE!

Brighton Masalu

MSALA! Kuna madai mazito yanayosema kuwa nyota wa filamu Bongo, Kajala Masanja ambaye alizaa na ‘prodyuza’ mkali wa muziki wa kizazi kipya, Paul Matthyssen ‘P Funk’ anamharibu mtoto wao anayefahamika kwa jina la Paula.
Nyota wa filamu Bongo, Kajala Masanja.
Chanzo ambacho pia ni rafiki wa karibu wa familia ya bosi huyo wa Bongo Records, kinasema wazazi hao hivi sasa wako katika mvutano mkubwa kutokana na kinachodaiwa kuwa mabadiliko ya tabia ya binti huyo mwenye umri wa miaka 13, anayesoma kidato cha kwanza katika shule moja iliyopo nje ya Jiji la Dar es Salaam.
Inadaiwa kuwa awali P Funk alikuwa akiishi na bintiye huyo, lakini Kajala hakukubaliana na suala hilo, hivyo akatumia mbinu alizojua na kufanikiwa kumchukua. Kwa ushauri wa marafiki zake, mtayarishaji huyo mtata, aliamua kumuachia mzazi mwenziye amlee, lakini kwa uangalizi wa karibu.
Baadaye, inadaiwa P Funk alianza kubaini mabadiliko kwa mwanaye, ikiwemo kujichanganya na makundi ya wasanii akiwa ameongozana na mama yake, kitu ambacho hakukipenda.
“Wakati anaishi kwa baba yake, Paula alikuwa na uwezo mzuri tu darasani, lakini sasa hivi, anavurunda kutokana na tabia anazofundishwa na mama yake, maana kila mahali alipo Kajala na huyo binti yupo, kwenye vikao na wasanii wa Bongo muvi, wakati mwingine usiku,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili lilimtafuta P Funk ili kusikia kauli yake kuhusiana na suala hilo, lakini licha ya kukiri kuwepo kwa tofauti kati yake na mzazi mwenzake juu ya malezi ya mtoto wao, alikataa kuingia kwa undani zaidi, akidai kuwa bize na kazi.
“Yule ni binti yangu, siwezi kuona anaharibikiwa na mimi nikakaa kimya, lazima nikemee, kwa hiyo utofauti upo, lakini kwa sasa sina nafasi ya kulizungumzia hilo,” alisema P- Funk.Risasi Mchanganyiko lilijaribu kuwasiliana na Kajala, lakini juhudi zake hazikuzaa matunda

DUA YAMUOKOA ASIUAWE

Dustan Shekidele, Morogoro.

SWADAKTA! Katika hali ya kustaajabisha, kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Ramadhan, ambaye mwishoni mwa wiki amejikuta akishushiwa kipigo kwa kudhaniwa kuwa kibaka, alisalimika baada ya kuanza kusali kwa kuwashtakia kwa Mwenyezi Mungu waliokuwa wakimpiga, akisema hakuwa na hatia na ghafla watu hao kusitisha kipigo.

Kijana Ramadhan akishusha dua zito baada ya kushushiwa kipigo kikali.
Ramadhan alikutana na hali hiyo baada ya kutuhumiwa kuiba redio kutoka katika duka moja lililopo stendi ya daladala mjini hapa.
Ilidaiwa kuwa kibaka huyo baada ya kuchukua redio hiyo alianza kukimbia kutokana na mwenye duka kumwitia mwizi na Ramadhan akawa mmoja kati ya watu waliokuwa wakimfukuza, kabla ya mdokozi huyo kujichanganya na watu hivyo kutotambulika kirahisi.
Baada ya kuona hivyo, wananchi hao wenye hasira walimgeukia kijana huyo na kuanza kumpa kipigo kama cha mbwa mwizi kwa vile nguo zake zilikuwa zimefanana na zile zilizokuwa zimevaliwa na kibaka aliyekuwa akifukuzwa.

....Akizidi kuomba.
”Ewe Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, kwa msaada wako niepushie na mtihani huu niliosingiziwa kwani wewe ndiwe unayejua ukweli wa tukio hili,” mtu huyo alisikika akisema kufuatia kipigo alichokuwa akikipata, baada ya kukimbia na kwenda kujibanza pembeni ya duka linalouza vinywaji baridi.
Kufuatia maneno hayo, watu wote walijikuta wakisitisha zoezi la kumpiga na mmoja wa bodaboda wa kijiwe cha Juwata aliingia kati na kusema; “Jamani huyu jamaa anaonekana siyo mwizi na ni mtu wa dini, hivyo naomba aliyeibiwa ajitokeze na kutoa ushuhuda,” alisema na hakuna aliyejitokeza.
Baada ya kuona hivyo, kijana huyo aliwataka watu hao kumuacha aende zake huku baadhi ya walioshiriki kumpiga wakimuomba msamaha mtu huyo aliyekuwa akivuja damu mwili mzima.Akizungumza na mwandishi wetu, Ramadhan alisema alishuka kwenye daladala na kuungana na watu waliokuwa wakimfukuza mwizi kabla hawajamgeuzia kibao kutokana na nguo zake kufanana na za kibaka.

Wananchi wenye hasira kali wakiwa eneo la tukio.
“Mwizi alijichanganya na watu ndipo nikageukiwa mimi, nikakimbilia hapa dukani kwa Mhindi na kuamua kuomba msaada kwa Mungu kwa kuomba na akafanikiwa kuniokoa,” alisema kijana huyo.
Katika stendi ya daladala, mfanyabiashara wa duka lililoibiwa, aliyejitambulisha kwa jina la Shaaban, alisema alikuwa amekwenda kutafuta chenchi, ndipo alipomuona mtu akiondoka na redio yake na yeye akapiga kelele za mwizi, akadondosha bidhaa hiyo na kukimbia, lakini akashindwa kuungana na watu kumkimbiza kwa vile hakukuwa na mtu mwingine dukani