Kijana
mfanyakazi wa ndani katika eneo la Kitwiru mjini Iringa
aliyefahamika kwa jina mmoja la Daniel mkazi wa mkoa wa Njombe
amekufa papo hapo baada ya kugongwa na daladala lililokuwa
likitokea mjini Iringa kwenda Mafinga wilaya ya Mufindi.
Wakizunguza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com na www.matukiodaima.com mashuhuda
wa tukio hilo wamesema kuwa kijana huyo aligongwa mida ya saa 2
usiku wakati akitoka kupeleka maziwa kwa mteja eneo la Ruaha na
wakati akirejea nyumbani ndipo alipogongwa na daladala hilo lililokuwa katika mwende kasi likitoka mjini Iringa kwenda Mafinga .
Hata hivyo walisema baada ya daladala hilo kumgonga halikuweza kusimama zaidi ya kuongeza mwendo na kuendelea na safari .
Pia walisema mwili wa kijana huyo ulikutwa na simu huku masikioni akionekana kuwa na vifaa maalum vya kumwezesha kusikiliza muziki kutoka katika simu na kuwa yawezekana ajali yake ilisababishwa na muziki aliokuwa akisikiliza kijana huyo na kushindwa kusikia honi ambavyo dereva wa daladala hilo alikuwa a
|
No comments:
Post a Comment