KESI
ya msanii wa filamu Bongo, Aisha Bui ya kufanya fujo ofisini kwa
msambazaji wa filamu akidai kutolipwa fedha zake za filamu bado ni ya
moto ambapo msambazaji anazungumza na mwanasheria wake kisha kumburuza
mwigizaji huyo mahakamani.Chanzo makini kimedai kuwa, baada ya Aisha kulala polisi na kutoka kwa dhamana msambazaji huyo, Ngeze Yuneda anatarajia kumburuza mahakamani akidai amembambikizia madai mengi ya uongo.
Alipoulizwa Aisha kuhusiana na habari hiyo, alisema:
“Hata sielewi kwa sababu walisema wanapeleka faili kwa mwanasheria ndipo tutakapoitwa ili ijulikane inakuwaje, nawasubiria.”
Aisha Bui akiwa mwenye gadhabu siku ya tukio.
Hivi karibuni Aisha alifanya fujo kwenye ofisi za Yuneda kutokana na
kumuuzia muvi tangu Aprili, mwaka huu lakini hakumpa fedha yoyote na
walikubaliana milioni tisa lakini alikuwa akimpiga kalenda ndipo
akamwangushia timbwili ofisini kwake.
No comments:
Post a Comment