
Wanaume nchini Kenya wameelezea
hisia mseto kuhusu wito wa kiongozi wa shirika la maendeleo la wanaume
nchini humo kwamba hii leo wasusie tendo la ndoa na kuonyesha hisia za
mapenzi kwa wanawake.
Wiki jana kiongozi huyo Nderitu Njoka
amewataka wanaume nchini Kenya kufanya hivyo kuadhimisha siku ya
kimataifa ya uhuru kwa wanaume inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 11
mwezi Novemba.Bwana Nderitu amewataka wanaume wote kutojihusisha na wanawake kimwili , wawe wameoa au la kama ishara ya kuonyesha ghadhabu yao kwa ongezeko la dhuluma wanazotendewa wanaume pamoja na ongezeko la utumiaji wa dawa za kulevya na pombe miongoni mwa wanawake.

Hatua hiyo pia inatumiwa kjuonyesha kero la wanaume kutokana na hatua ya serikali kutenga shilingi bilioni mbili kwa mahitaji ya wasichana wakati ikikosa kutoa mchango kama huo katika kusadia wanaume wengi kufanyiwa tohara.
Njoka alinukuliwa akisema kuwa kidini wanaume ndio viongozi wa familia lakini leo wamedhalilishwa huku wanawake wakitawala dunia.
No comments:
Post a Comment