
“Ngozi yake kuonekana kama ya mzee huku macho yake yakionekana kuwa makubwa na kichwa chake kuwa na umbo la nyoka pamoja na miguu, baada ya kuona hali hii tukaihusisha na mambo ya kishirikina na kuamua kuanza maombi,
Mtoto mchanga mwenye umri wa miezi minne amezua kizaazaa cha aina
yake, baada ya kuwapo taarifa kwamba mara kadhaa umbo lake limekuwa
likigeuka na kuwa nyoka na mwili wake ukiendelea kudhoofu kutokana na
kukataa kunyonya maziwa ya mama yake.
Mtoto huyo (jina lake tunalihifadhi kwa sasa), wiki iliyopita alivuta
umati wa wakazi wa Kijiji cha Nkome mkoani Geita ambao walifurika ndani
na nje ya Kanisa la AICT Nkome, lililopo kijiji hapo,
kushuhudia maombi ambayo alikuwa akifanyiwa ili kumkomboa katika kile
kilichotafsiriwa kuwa ni mateso dhidi yake.
Ilikuwa saa 4.00 asubuhi Jumamosi, Novemba 8 mwaka huu wakati mtoto
huyo alipofikishwa katika kanisa hilo na kuanza kufanyiwa maombi na
sababu ya hatua hiyo ikielezwa kuwa ni kutokana na kuwa na umbo la nyoka
na kwamba matendo yake yanaashiria kwamba mwenye asili ya nyoka ndani
ya roho yake.
Mtoto huyo alifikishwa kanisani hapo na mama yake mzazi, Sarah Silasi
wakitokea Kijiji cha Ichile, Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, ambako
alikimbia matukio yanayohusishwa na ushirikina.
Mmoja wa wazee wa kanisa hilo la AIC Nkome, Mathew Misana anasema: “Alikuwa
anatoa ulimi mithili ya nyoka, mwendo wake anapolala alijizungusha kama
nyoka na hata alipojikunja mwili wake ulikuwa kama unavyoona nyoka.”
Misana anasema matukio hayo na mengine kadhaa yakiwamo ya ngozi ya
mtoto huyo kuwa nyeusi kama ya nyoka aina ya chatu, yaliwalazimisha
ndugu na jamaa zake wakiongozwa na mama mzazi kutaka aombewe.
No comments:
Post a Comment