pia
ni mwimba Injili, Sara Mvungi anateseka hospitalini baada ya
kusumbuliwa mara kwa mara na ugonjwa wa nimonia (pneumonia) ambao
umekuwa ukimkosesha amani na muda wa kufanya kazi za kimaendeleo.
Akizungumza kwa taabu na Ijumaa Wikienda akiwa amelazwa kwenye
Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni jijini Dar, Sara alisema kuwa ugonjwa
huo umekuwa ukimtesa hata kusipokuwa na baridi kutokana na hali ya hewa
ambayo haieleweki.
“Jamani kama ni kwa sababu ya baridi ndiyo
maana naumwa kiasi hiki hata siamini kwani hata kipindi cha joto,
najikuta naumwa ugonjwa huu,” alisema Sara akionekana kuwa na maumivu
makali.
Sara aliongeza kwamba, anamshukuru Mungu na ni mwema kuona sasa anaweza kupumua kwani hali yake ilikuwa mbaya kwa kuwa ugonjwa huo uliambatana na malaria kali.
Hata hivyo, Sara aliwashukuru wasanii waliokuwa wakifika hospitalini
hapo kumuona na Watanzania wote wanaomuombea na anawasihi wazidi
kumuombea. Sara amewahi kuripotiwa na gazeti hili kulazwa kwenye
hospitali hiyohiyo ya TMJ akisumbuliwa na ugonjwa huohuo hali
inayosababisha mashabiki wake kuhoji kwa nini ugonjwa huo umekuwa
ukimsumbua na wengine kumshauri kuhakikisha anautibu na kumaliza tatizo
hiloSara aliongeza kwamba, anamshukuru Mungu na ni mwema kuona sasa anaweza kupumua kwani hali yake ilikuwa mbaya kwa kuwa ugonjwa huo uliambatana na malaria kali.

No comments:
Post a Comment