Wakazi wa Majohe Kichangani wakiomboleza msiba wa mtoto Nuru Mohamed (7)
nyumbani kwa wazazi wa marehemu, Dar es Salaam jana. Picha na Daria
Erasto.
Na Daria Erasto,Mwananchi
Posted Jumatano,Novemba12 2014 saa 9:12 AM

Kwa ufupi
Alipotea kwa siku sita kabla ya maiti kukutwa imefunikwa kwa matofali katika jumba ambalo halijakamilika ujenzi eneo la Majohe.
Dar es Salaam. Mtoto Nuru
Mohamedi (7) ameuawa kikatili na kisha mwili wake kutelekezwa kwenye
nyumba ambayo haijakamilika ujenzi iliyo Majohe Kichangani mjini hapa.
Tukio hilo, ambalo limezua hofu na huzuni kwa wakazi wa mtaa huo, lilibainika jana baada ya kupatikana kwa maiti ya mtoto huyo ambaye kabla ya mauti kumkuta alikuwa amepotea katika mazingira ya kutatanisha tangu Novemba 6.Akisimulia tukio hilo kwa tabu huku akilia kwa huzuni, mama mzazi wa mtoto huyo, Sauda Ally alisema Alhamisi iliyopita saa 1:00 usiku mtoto wake alikuwa akicheza nje ya nyumba yao pa
“Baadaye akaja mtoto wa jirani aitwaye Dula, akaniambia Nuru amekwenda na babu mmoja alimwambia amsindikize dukani, nilinyanyuka haraka na kutoka nje na kuanza kumwita, lakini hakuitika,” alisema.
Alisema baada ya kuona hali hiyo alikimbia hadi dukani alikoelekezwa kuwa mwanaye amekwenda, lakini hakumwona hivyo aliamua kuomba msaada kwa majirani na taarifa zilipelekwa katika msikiti wa karibu kwa ajili ya kutangazwa na kisha waliendelea kutoa taarifa hizo kituo cha polisi cha Gongo la Mboto.
Alisema mtoto wake alitafutwa bila mafanikio kwa siku sita.
Alisema, jana asubuhi mmoja wa wapangaji wake alipokea simu kutoka kwa jirani yake anayeishi eneo la Kwa Mkandawile kwamba kuna maiti ya mtoto imeonekana katika maeneo hayo na kwamba huenda akawa ni mtoto wake.
Hata hivyo, Sauda alishindwa kuelezea zaidi mkasa huo na mama mkubwa wa marehemu, Rehema Ally alisema kuwa baada ya simu hiyo waliondoka mara moja kwenda eneo la tukio.
“Tuliona maiti ya mtoto ikiwa imefukiwa kwa matofali na sehemu ya kichwa ikiwa imebaki nje”.
“Kwa kweli hali tuliyoikuta ilikuwa inatisha. Alikuwa amefunikwa kwa matofali, upande wa kisogoni tu ndiyo ulikuwa ukionekana. Tulitoa taarifa polisi na walipofika, waliinyanyua na ndipo tulipothibitisha maiti ile ilikuwa ya Nuru na alikuwa amevuliwa nguo zote.”
Alisema watekelezaji wa tukio hilo walifanya ukatili wa hali ya juu, kwani baada ya uchunguzi wa daktari ilibainika kuwa na majeraha katika sehemu ya paja, lililokuwa na tundu lililofunikwa kwa plasta na kisogoni ilionekana amepigwa na kitu kama jiwe.
Alisema anasikitishwa na kitendo cha kuuawa kinyama na kudhalilishwa alichofanyiwa mtoto wao, kwani kinaonyesha kushuka kwa hali ya usalama wa watoto na kuitaka polisi kuhakikisha inachunguza kwa undani taarifa za utekaji watoto na si kuzipuuzia.
moja na watoto wengine wawili.

No comments:
Post a Comment