WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Usevya, wilayani Mlele, Katavi,
wamezishambulia familia mbili kwa kutumia silaha za jadi na kuwavunjia nyumba
zao baada ya kuzituhumu kujihusisha na vitendo vya kishirikina na kusababusha
kifo cha mwalimu wao Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari,
alisema jana kuwa tukio hili lilitokea juzi, majira ya saa 12 alfajiri baada ya
wanafunzi hao kupata taarifa ya kifo cha mwalimu wao, Tumsifu Philimon (28)
katika Hospitali ya Sumbawanga alikokuwa akipatiwa matibabu.
Kidavashari aliwataja waliovamiwa nyumba zao na wanafunzi hao ni Philipo
Mwanjisi na Aprotina Mkalala ambapo mbali ya nyumba zao kuvunjwa walishambuliwa
kwa kupigwa na mawe.
Kabla ya tukio hilo,
mmoja wa familia hizo alifika shuleni hapo wiki iliyopita kwa lengo la kuonana
na Mwalimu Tumsifu baada ya kupata malalamiko kutoka kwa mtoto wake aliyekuwa
akisoma hapo kuwa amepigwa viboko na mwalimu huyo.
Inadaiwa baada ya mzazi huyo kufika shuleni hapo alimpa vitisho mwalimu huyo
huku baadhi ya wanafunzi wakisikia vitisho vilivyotolewa na mzazi huyo.
Siku iliyofuata mwalimu huyo aliamka anaumwa na ndipo alipokwenda Sumbawanga
kwa matibabu na April 12 alitoweka hospitalini hapo; na Aprili 15 alikutwa
amekufa kandokando mwa mto huku akiwa amenyofolewa macho.
Kamanda Kidavashari alisema wanafunzi hao walihisi kifo cha mwalimu wao
kimesababishwa na ushirikina wa wanakijiji hao wawili na ndipo walipokwenda
kuwashambulia.
Alisema upelelezi wa tukio hilo
unaendelea na wanafunzi watakaobainika kuhusika watachukuliwa hatua.

No comments:
Post a Comment