airport jogging

mavazi

aus521

aus9

Sunday, November 30, 2014

WASTARA AKANA KUCHUMBIWA

Stori: Hamida Hassan
STAA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma, amepinga vikali taarifa kuwa ametolewa posa na msanii mwenzake, Bond Bin Sinan  na kusema kuwa kwa sasa hahitaji kuchumbiwa, wala bwana kwani hajaamua kwenda huko.
Staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma.
Akikitendea haki kipaza sauti cha Ijumaa Wikienda, Wastara alisema anaona kuwa aliyeeneza habari hizo anamuwangia kwani hana wazo la kuchumbiwa kwa sasa.
“Sitaki kuolewa wala kuchumbiwa, wala bwana bado sijaamua kwenda huko,” alisema Wastara ambaye amekuwa akipinga vikali kuwa na uhusiano Bond licha ya kuonekana naye kwenye pozi tata mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment