Kama kawaida Ijumaa iliyopita mapaparazi wetu wanaotii amri ya bosi wao, Richard Bukos ‘Mpiga Picha Mkuu’, Issa Mnally ‘Mzee wa GX 100,’ Shani Ramadhani ‘Mamaa Libeneke’na Dustan Shekidele ‘Mkude Simba’ walisambaa kwenye viwanja tofauti vya burudani huku wakiwasiliana moja kwa moja na mkuu wao aliyekuwa makao makuu ya ofisi za gazeti hili, Bamaga- Mwenge, jijini Dar.
Mkuu akiwa katika kiti chake cha kujidai, anameza funda la mwisho la kahawa, anaangalia saa na kugundua kuwa tayari ni saa nne kamili na kuanza kumtafuta Bukos.
Saa 5:20 usiku
Changu agombana na mteja
Makao Makuu: Shani Ramadhani ‘Mamaa Libeneke’ haya kazi kwako, nipe ripoti upo maeneo gani muda huu?

Shani: Mkuu nipo maeneo ya Sinza Afrikasana kuna changu anagombana na mteja wake, kisa hajalipwa pesa yake.
Makao Makuu: Imekuwaje sasa?
Shani: Wamekusanyika machangu kibao kumsaidia mwenzao alipwe ujira wake mpaka kalipwa.
Makao Makuu: Sawasawa endelea kupiga kazi.

Watoto wa mbwa watibua harusi ya mwanamuziki wa Yamoto Band
Bukos: Mkuu niko maeneo ya Kinondoni nakaribia kabisa Ukumbi wa Vijana lakini kuna dada mmoja amenipigia simu ananiambia yuko Temeke Vetenary kwenye harusi ya mwanamuziki wa Yamoto Band, anaitwa Abdallah Kiambwe almaarufu kama Dulla Yeyo leo lilitokea bonge la varangati.
Makao Makuu: Ilikuwaje?

Bukos: Mkuu huyo mdada amesema nisimtaje jina lake gazetini lakini amesema chanzo ni masela tu wa mtaani maarufu kwa jina la watoto wa mbwa walilewa ndiyo wakaamua kufanya vurugu.
Makao Makuu: Amesema ni madhara gani yametokea?

Bukos: Mkuu sijapata tathmini ya hasara iliyopatikana isipokuwa Yamoto Band walitaka kutumbuiza kwenye hiyo harusi lakini baada ya vurugu wameshindwa.
Makao Makuu: Dah! Naomba fanya juu chini umpigie Mkubwa Fella na Wanae akupe habari kamili.
Bukos: Mkuu nimeshampigia zaidi ya mara kumi lakini naambiwa simu yake haipatikani si unajua hii mitandao yetu kuna wakati inazingua!

Makao Makuu: Aisee ni noma sana.
Saa 6:13 usiku
Masangula wa Msongola akiona cha moto
Makao Makuu: Issa Mnally Mzee wa ‘GX 100’ upo pande zipi?
Mnally: Kiongozi mimi leo nipo nje kidogo ya Jiji la Dar, pande za Msongola Mbagala ndani ya Ukumbi wa burudani wa Santiago.

Makao Makuu: Duu! Umefuata nini huko?
Mnally: Mkuu hapa ukumbini kuna Kundi la Mnanda la Survivor linafanya yake, kiongozi acha kabisa pana vituko vya ajabu usipime.

Makao Makuu: Ahaaa nafahamu sana sehemu ambayo kunakuwa na Mnanda mambo yanavyokuwa, nijuze baadhi ya vituko hivyo.
Mnally: Mkuu, kuna akina dada wanakata mauno huku wakiwa nusu utupu na pombe za aina zote zinanywewa yaani ulaka, kangara, mnazi na bia.
Makao Makuu: Vipi umewalamba picha?
Mmally: Za kumwaga Mkuu.

Makao Makuu: Kuna tukio gani lingine umelinasa?
Mnally: Mkuu Mkurugenzi wa ukumbi huu, Selemani Masangula amekiona cha moto baada ya kupigwa na kiti cha kichwa na shabiki mmoja.
Makao Makuu: Kisa nini cha kufanyiwa unyambilisi huo?
Mnally: Nasikia aliwabania masela kutinga ukumbini.
Makao Makuu: Duuuh! Hiyo kali, Oke Mnally nitakupigia baadaye kujua kitakachojiri tena hapo.
Mnally: Sawa Mkuu.

Saa 7:08 usiku
Mshiriki karusha mshale kwa jazba mpaka umevunjika
Makao Makuu: Halooo...halooo...we Shekidele simu yako leo kimeo, kwa nini nakupigia muda wote hupatikani?

Shekidele: Samahani Mkuu simu yangu ina tatizo inazimazima tu.
Makao Makuu: Haya haraka niambie uko wapi na kitu gani kinaendelea.
Shekidele: Mkuu mwanzo nilikuwa pande za Midizini Pub kwenye ukumbi unaomilikiwa na Afisa wa Polisi, Salum Likukwara kuna shindano la kurusha mishale (Dats) upinzani ni mkali sana.
Makao Makuu: Enhe imekuwaje?

Shekidele: Kuna mshiriki mmoja kwa jazba karusha mshale kwa nguvu kwa lengo la kusaka ushindi matokeo yake kauvunja.
Makao Makuu: Dah hiyo balaa kwa hiyo sasa hivi uko wapi?
Shekidele: Nipo Kihonda Mkuu kuna rafiki yangu ni Kanali wa Jeshi anaitwa Mayao alinipa taarifa kuwa mtaa wa Godes Kihonda kuna mchawi kadondoka sasa wananchi wa maeneo haya wameshikwa na taharuki kila kukicha mambo ya kishirikina yanatokea.

Makao Makuu: Kwa hiyo umefika eneo la tukio?
Shekidele: Nimefika fasta Mkuu na nimemshuhudia mchawi huyo akiwa mtupu bila nguo.
Makao Makuu: Safi jitahidi utoke hapo na uwapigie simu wenzako, waambie mkapumzike na suala la kuwahi kazini kesho asubuhi ni kama jadi.
Shikidele: Sawa Mkuu wangu

No comments:
Post a Comment