airport jogging

mavazi

aus521

aus9

Monday, November 10, 2014

Wema Sepetu na Penny wamaliza tofauti zao, wakumbatiana na kupiga picha pamoja 
 

Hatimaye mpenzi wa sasa (Wema) na mpenzi wa zamani (Penny) wa msanii wa Bongo fleva Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz wamemaliza tofauti zao zilizotokana na ‘penzi’ la hit maker huyo wa ‘Number 1’.

Muigizaji wa Bongo Movie Wema Sepetu na mtangazaji wa E-FM Penny Mungilwa a.k.a VJ Penny walikutana usiku wa jana kwenye birthday dinner ya rafiki yao aitwaye Junaithar ambaye ndiye aliyewapatanisha.

Picha za Wema na Penny wakikumbatiana huku nyuso zao zikiwa na tabasamu zimeashiria kuwa sasa kila mmoja ameacha yaliyopita na hana kinyongo na mwenzake.

Kupitia Instagram Junaithar aliyewapatanisha aliandika:
“Wema na penny leo wamemaliza tofauti zao nilijuwa wema kupitaa penny nawapenda sana wadogo zangu @wemasepetu_auntyezekiel @vjpenny04 @nsepetu”
Picha: Instagram

No comments:

Post a Comment