airport jogging

mavazi

aus521

aus9

Tuesday, December 16, 2014

AISHA, LILI WAIBUKA NA KUSEMA TUMEKUZA

Stori: Imelda Mtema
WASANII wakongwe waliotamba ndani ya kundi la Nyota Ensamble, Theckla Mgaya ‘Aisha’ na Leilah Mohamed ‘Lili’ wameibuka na kusema kuwa wamekuza, baada ya kushuhudia watoto wao wakimaliza kidato cha nne katika shule mbili tofauti jijini Dar es Salaam.
Msanii mkongwe wa kundi la Nyota Ensamble, Leilah Mohamed ‘Lili’akiwa na mwanaye.
Tarzan Msenga, mtoto wa kiume wa Aisha, alihitimu kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Royola wakati kijana wa Lili, aitwaye Rahim, aliyezaa na muigizaji mwenzake Jumanne Kihangala ‘Mr Chuz’ yeye alihitimu elimu hiyo katika shule ya Green Acres.
“Ni Mungu ndiye wa kushukuriwa kwa kila jambo kwa maana amefanya mambo mazuri kwa mwanangu na hivi sasa mimi nimekuza kabisa,” alisema Aisha huku mwenzake Lili akilalamika kwa kitendo cha mzazi mwenzake kutomsaidia kwa lolote hivyo kujikuta akiifanya kazi hiyo peke yake.
Msanii mkongwe wa kundi la Nyota Ensamble, Theckla Mgaya ‘Aisha’ akiwa na mwanaye.
“ Yaani mtoto wangu nimemlea kwa tabu sana, ukizingatia baba yake tangu zamani hana habari kabisa hivyo kufikia hapo alipo ni Mungu na azidi kumkuza siku zote,” alisema Lili.

No comments:

Post a Comment