Na Gladness MallyaMSANII wa filamu Bongo, Shamsa Ford hivi karibuni alijikuta akiangua kilio uwanjani baada ya timu yake anayoishabikia ya Yanga kufungwa mabao mawili bila.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Taifa ambapo kulikuwa na mechi ya Nani Mtani Jembe 2 iliyozichezesha timu za Simba na Yanga ambapo Shamsa alijikuta akilia kama mtoto baada ya timu yake kufungwa mabao 2-0.
“Unajua mimi ni Yanga damdam kufungwa imeniuma sana na nilishindwa kabisa kujizuia machozi, ukweli Yanga wanatukosea sana wao hawajui tu kwamba sisi mashabiki zao tunaumia,” alisema Shamsa.

No comments:
Post a Comment