airport jogging

mavazi

aus521

aus9

Wednesday, April 15, 2015

ALA KICHAPO KISA MUME WA MTU

aus9
Dada mmoja aliyefahamika kwa jina la Jamila mkazi wa Kawe jijini Dar hivi karibuni alipata kipigo cha kufa mtu akituhumiwa kuchepuka na mume wa mwanamke mmoja aitwaye Sheila.Tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo ilielezwa kuwa, Sheila alitonywa na wambeya kuwa Jamila amekuwa akichepuka na mumewe na bila kuchunguza akapanga kumshikisha adabu.
Jamila akiwa na jeraha usoni kwa tuhuma zakutembea na mume wa mtu.
“Jamila alikuwa akituhumiwa kutembea na mume wa Sheila na siku ya tukio alifuatwa baa na kupigwa hadi kutaka kutobolewa jicho,” kilidai chanzo.
Mwandishi wetu alifanya jitihada za kuwatafuta wahusika ambapo Jamila alipopatikana alisema:
 “Jamani ukweli ni kwamba mimi niliwahi kutembea na yule mume wa Sheila lakini tulishaachana sasa nimemshangaa mkewe kuja na kunipa kipigo sababu tu ya maneno ya kusikia”, alisema Jamila na kuongeza:
Mwenye mume.
“Nilikwenda kufungua kesi Kituo cha Polisi Kawe lakini siku chache baadaye Sheila alikuja na kuniomba msamaha akidai kuwa alikosea kuamini maneno ya watu bila kufanya uchunguzi. Tumesameheana na yameisha

No comments:

Post a Comment