UBABE? WASANII katika tasnia ya filamu, Irene Paul ‘Smart
Girl’ na Halima Yahaya ‘Davina’ wamejikuta wakitaka kuzichapa kavukavu
baada ya kushindwa kudhibiti hasira walipokuwa wakitaniana.
Ishu hiyo ilitokea juzikati ndani ya Viwanja vya Leaders Club,
Kinondoni jijini Dar, kulipokuwa na mkusanyiko wa wasanii mbalimbali
ndipo wawili hao walipotunishiana misuli.
Ishu hiyo iliibuka baada ya Davina kumtupia maneno ya kejeli mwenzake
huku Irene akionekana kuwa ‘siriaz’ akitahadharisha kuwa hapendi utani
na kuanza kumtupia maneno makali jambo lililowafanya baadhi ya wasanii
kutuliza hali ya hewa.
Mwandishi wetu aliyeshuhudia tukio hilo mita chache na mahali
alipokuwa, alishuhudia Davina naye akimpa maneno makali mwenzake ndipo
wakataka kuzichapa lakini bahati nzuri wakaamuliwa
No comments:
Post a Comment