Habari kutoka chanzo cha kuaminika ambacho ni ndugu wa Siwema kilieleza kuwa, pamoja na maneno ya shombo aliyommwagia Nay wakati wanaachana, mrembo huyo kwa sasa ameweka silaha chini akiomba wawe kama zamani.
Kilidai kwamba hivi karibuni, mmoja wa dada wa Siwema (jina linahifadhiwa) amekuwa akimpigia simu Nay akimuomba arudishe moyo wake kwa Siwema, kwani tangu aachane naye mambo yamekuwa yakienda kombo ikiwemo ule msala wa kesi inayoendelea mahakamani ya kujipatia mali isivyo kihalali.

Ney wa mitego , Siwema Edson wakiwa na mtoto wao.
Baada ya kumwagiwa ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilituma kijumbe
kumfikishia Nay ombi hilo la Siwema ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Kweli nimepokea simu za msamaha. Nimemsamehe lakini siwezi kurudiana
naye.”Kwa upande wake mama Nay alisema yeye ndiye alikuwa mtetezi wake lakini kwa sasa hataki kusikia ishu hiyo.
No comments:
Post a Comment