Dustan Shekidele, Morogoro.LAANA! Njemba mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, anayejishughulisha na ujenzi wa nyumba, mwishoni mwa wiki alinaswa kwa tuhuma za kumbaka mtoto mdogo wa kike (10) katika nyumba aliyokuwa akiijenga maeneo ya Kichangani mkoani hapa, Risasi Mchanganyiko linakujuza.
Mtuhumiwa huyo akiwa chini ya ulinzi.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mtoto huyo ambaye jina lake
linahifadhiwa, alikuwa akienda kununua maziwa mtaa wa pili, ndipo jamaa
huyo alipomuita ndani ya nyumba hiyo na kufanikiwa kumbaka akiwa
amemziba mdomo, kumzuia asipige kelele.
....Akitolewa katika kituo cha polisi.
Inadaiwa kuwa baada ya kumaliza kufanya kitendo hicho, mtoto huyo
aliendelea na safari yake ya kununua maziwa, lakini aliporejea nyumbani,
mama yake aligundua hali isiyo ya kawaida hivyo kumuuliza nini
kilimsibu.“Ndipo huyo binti akamwambia mama yake kuwa alipokuwa akienda kununua maziwa, aliitwa na huyo fundi na kufanyiwa kitendo kibaya, jambo ambalo lilimfanya mama huyo kumchukua mwanaye na kumpeleka polisi, ambako walishauriwa kwenda hospitalini kwanza na huko ikathibitika kuwa kweli alibakwa,” alisema shuhuda huyo.
No comments:
Post a Comment