Kikongwe Kete Abdallah aliyemtabilia Magufuli.
Dustan Shekidele, Morogoro.UTABIRI! Wakati taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali zikitoa matokeo ya utafiti katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu mwezi ujao, kikongwe mmoja, Kete Abdallah mwenye umri wa miaka 100, amemtabiria ushindi mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli.
Akikata keki kwenye siku yake ya kuzaliwa.
Bibi huyo alitoa utabiri huo wiki iliyopita wakati wa sherehe yake ya
kumbukumbu ya kuzaliwa iliyoandaliwa na wajukuu na vilembwe wake na
kufanyika nyumbani kwake, Ukonga jijini Dar es Salaam.Mmoja wa wajukuu
zake, Dustan Shekidele ambaye ni mwandishi wa gazeti hili, alisema
alimkuta bibi yake akiwa amelala kitandani akiwa amekumbatia redio na
alipomuuliza sababu ya kuwa hivyo, alidai anafuatilia habari za mgombea
huyo, kwani anaamini atashinda na endapo ataamka salama siku hiyo,
atampatia kura yake ya ndiyo.
...Akimlisha mwanaye keki.
"Unajua ukubwa dawa, najua kila mtu ana chama chake siwezi
kuwaingilia, lakini ninawashauri viongozi wangu wa CCM, uchaguzi wa
mwaka huu ni mgumu, upinzani umekuwa na nguvu,” alisema bibi huyo na
kuwashauri viongozi wa CCM kutembelea majumbani na mahospitalini
kuwabaini makada wa CCM ambao hawataweza kutoka kwenda kupiga kura.Mmoja wa vilembwe wa bibi huyo, Tumaini Shekidele akisoma risala kwenye sherehe hiyo, alisema bibi huyo alizaliwa Septemba 27, 1915 katika Tarafa ya Mlalo Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga na kwamba hadi sasa ana wajukuu na vilembwe 302.
No comments:
Post a Comment