Vanessa Mdee alitumbuiza kwenye show ya mkesha wa mwaka mpya nchini
Malawi, mwishoni mwa wiki. Lakini hakuishia tu kutumbuiza, bali alitumia
muda huo kurekodi wimbo anaoshirikishwa na rapper wa nchini humo, Tay
Grin.

Kwa muda mrefu Tay alikuwa akidai kuwa anapenda aje arekodi wimbo na
muimbaji huyo wa Cash Madame, na sasa fursa hiyo imepatikana hatimaye.

Vee na Tay wameshare picha kadhaa za studio session yao kwenye Instagram.
“Studio session! @vanessamdee @sonyezo and yours truly. The fire levels on this song is on the higher side. CANT wait for y’all to hear it. Too much
,” ameandik Tay.

Mwaka jana Tay aliiambia Bongo5: Napenda jinsi wasanii wa
Tanzania wanavyoimba. Ni kimuziki sana hata kama sizungumzii Kiswahili,
muziki wao unasikika vizuri na ni mtamu. Nimesikiliza wasanii kama
Vanessa Mdee, Diamond Platnumz, Alikiba na muziki wao wa Bongo Flava.
Nadhani Nyau Music inaweza kuchanganyikana vizuri na wasanii hawa
wakali. Kwa sasa ninafanyia kazi wimbo na Vanessa Mdee na nina matumani
ya kumpata Diamond Platnumz kwenye wimbo huo

Vanessa Mdee akiingiza sauti kwenye booth

Vee na Tay wameshare picha kadhaa za studio session yao kwenye Instagram.
“Studio session! @vanessamdee @sonyezo and yours truly. The fire levels on this song is on the higher side. CANT wait for y’all to hear it. Too much

Vanessa Mdee akiwa amejilaza kwenye kochi wakati Tay Grin akiingiza sauti zake
No comments:
Post a Comment