airport jogging

mavazi

aus521

aus9

Tuesday, May 31, 2016

Prezzo amfuata Gigy Bongo!

Prezzo
IMEVUJA! Kumbe rapa mwenye jina kubwa Afrika Mashariki, Jackson Makini ‘Prezzo’moja ya ishu zilizomleta Bongo ni pamoja na kukutana na muuza nyago kwenye Video za Kibongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’.
Gigy Money
Akichonga na mtandao huu, Prezzo aliyewahi kubamba na Ngoma ya Nipe Nikupe akimshirikisha staa wa Bongo Fleva, Ambwene Yessaya ‘AY’ alisema kuwa, Gigy ni msichana ambaye amekuwa akimsikia siku za hivi karibuni Wakenya wakimzungumzia hasa juu ya vituko vyake jambo lililomfanya kuvutiwa kuonana naye.
“Gigy yuko hot mazee, nimemsikia sana Wakenya wakimzungumzia so nipo katika mpango wa kuonana naye, si unajua mimi nina mambo mengi, reality show na vitu vingine private,” alisema Prezzo. Gigy Money aliponyetishiwa ishu hiyo alifurahia jina lake kupaa hadi Kenya.

Baada ya Nay Kuchepuka… Lulu Diva Amgeukia Belle 9

lulu la diva (6)Lulu Diva
SIYO siri tena! Baada ya mkali wa Muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kuchepuka kwa msichana wa Kihabeshi mwenye asili ya Ethiopia, aliyekuwa mpenzi wake Lulu Abass ‘Lulu Diva’ naye ameamua kugeukia kwa staa wa muziki, Abedinego Damian ‘Belle 9’.
belle91Belle 9
Akizungumza na Over Ze Weekend Lulu ambaye ni muuza nyago kwenye video za Kibongo alidai kuwa, Nay hajatulia na badala yake anahitaji kuwa na mtu asiye na skendo za kutembea na wanawake ovyo na Belle 9 ndiye tulizo lake.
“Ni ukweli Nay nilikuwa naye kwenye uhusiano nikifahamu alishawahi kuwa na msururu wa wanawake lakini siyo siri yamenishinda na sasa nahitaji kujiweka kando. Sasa hivi feelings zangu zote zipo kwa Belle na analijua hilo,” alisema Lulu.

Kidoa Alamba Shavu la Kutangaza Nguo EBM

kidoa

STORI: HAMIDA HASSAN, WIKIENDA
VIDEO Queen Asha Salum ‘Kidoa’ hivi karibuni ameibua maswali mengi mtandaoni baada ya kutupia picha akiwa ameonesha nguo ya ndani ambapo wengi wamemkejeli kwa picha hizo.

Lungi alinanga penzi la Wolper, Harmonize

Harmonizer-na-Wolper 
Jacqueline Wolper na Rajab Abdulhan ‘Harmonize’
STORI: HAMIDA HASSAN, WIKIENDA
MSANII wa filamu wa kitambo, Lungi Maulanga amelinanga penzi na Jacqueline Wolper na Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ akisema kuwa, anachoona ni kama Wolper anatembea na mdogo wake.
LUNGI (1)Lungi Maulanga
Akiuzungumzia uhusiano wa mastaa hao, Lungi alisema alijisikia vibaya sana kuona shosti wake Wolper kafa, kaoza kwa Harmonize kutokana na tofauti kubwa iliyopo kati yao.
“Unajua Wolper ni kama mdogo wangu na shosti wangu hivyo siwezi kumuacha apotee, mimi nitamuita tutaongea kwa kina, kama atashikilia msimamo wake nitamuacha kwa sababu si unajua mtu akishapenda, lakini kiukweli hawajaendana,” alisema Lungi

Ishu Ya Kuchoropoa Mimba, Wema Kumfunga Jela Harmonize

WEMA2Wema Isaac Sepetu ‘Madam’
STORI: Mwandishi Wetu, Ijumaa
Dar es Salaam: Endapo mkali wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ atalivalia njuga suala la kudhalilishwa mtandaoni na msanii aliye chini ya Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Rajab Abdulhan ‘Harmonize’, jamaa huyo atakwenda jela miaka kadhaa na faini juu.
harmonize kasuku - bekaboyRajab Abdulhan ‘Harmonize’
CHANZO NI NINI?
Juzikati, Harmonize au Hamo, akiwa na kundi la wasanii wenzake katika eneo ambalo halikujulikana ni wapi, walijichukua clip (kipande cha video) kwa staili ya kujipiga ‘selfie’ huku Harmonize akiimba wimbo wa msanii Stamina uitwao Mwambie Mwenzio, ambao kwenye mistari hiyo dogo huyo alisherehesha kwa kusema kuwa, usitoe mimba usije ukaja kulia kama (Wema) Sepetu.
HARMONIZE ALA ZA USO
Baada ya Harmonize kuwaongoza vijana hao kumdhalilisha Wema kwa staili hiyo, watu wengi kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii walimpa jamaa huyo za uso, baadhi wakisema kuwa, umaarufu mdogo alioupata unamzuzua.
Wema SepetuWema na mama yake mzazi.
“Huyu mtoto anaona ameshakuwa maarufu sasa, anaona sawa kuwatukana hata wakubwa zake au ametumwa?” alihoji mmoja wa mashabiki wa Wema (Team Wema) aliyejitambulisha kwa jina la C_K kwenye Mtandao wa Instagram.
Mwingine akaandika: “Ninachojua huyu dogo anatafuta kiki lakini siyo kwa kufanya mambo haya, hivi ana ushahidi gani kama Wema katoa mimba?”
Harmonizer-na-Wolper 
Harmonize na Wolper
KAULI YA TCRA
Akizungumzia sakata hilo, Afisa kutoka Dawati la Malalamiko wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Doris Mhimbira alisema kuwa ni kosa la jinai ambalo mlalamikaji akiwa ‘serious’ anaweza kusababisha Harmonize akachukuliwa hatua kali za kisheria.

Tuesday, December 29, 2015

PATA LINK YA SHOE YA DAIMOND DAR LIVE....

Davido na Tekno wanachangia penzi la Masogange?


Aggy31Agnes Masogange.
RIPOTI zimesambaa kwamba wanamuziki nyota wawili wa Nigeria, Davido na Tekno, huenda wanachangia penzi la mrembo wa Kitanzania, Agnes Masogange.
Mwezi Novemba mwaka huu mwimbaji Davido ambaye alivuma na album ya Omo Baba Olowo (Mtoto wa Tajiri) alijirusha na wasichana kadhaa wakati wa bethidei yake na mmoja wao alikuwa Masogane na baadaye zikaenea habari kwamba alikuwa mjamzito akitegemewa kumzalia Davido mtoto wa pili, lakini habari hizo baadaye zikakanushwa.
image (5)…..Akiwa na Tecno.
Kitu cha ajabu ni kwamba Masogange alianza kuweka na kufuta ujumbe mbalimbali kwenye mtandao ukionyesha alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Tekno kwa kula naye bata katika hoteli moja nchini Afrika Kusini.
Agnes-na-DavidoTekno naye alianza kutuma ujumbe kama huo, jambo lililowafanya mashabiki wake kuamini alikuwa na uhusiano na msichana huyo. Hata hivyo, mwimbaji huyo ameufuta ujumbe wote huo katika ukurasa wake

Tiwa Savage awashangaza mashabiki kuvaa gauni la guniaTiwa Savage awashangaza mashabiki kuvaa gauni la gunia


Tiwa-Savage-headies-600x600Mwanamuziki machachari wa Nigeria, Tiwa Savage.
MWANAMUZIKI machachari wa Nigeria, Tiwa Savage, majuzi aliwashangaza mashabiki wake kwa kuvaa gauni la gunia kwenye hafla ya fasheni ya kampuni ya prodyuza ya Marvin Records.
image (4)….Akiwa amevaa gunia.
Bila kujali macho na maneno ya watu, nyota huyo mwenye mtoto mmoja alitinga katika hafla hiyo iliyokwenda kwa jina la One Lagos Concert iliyofanyika eneo la Ikorodu akiwa ‘ng’aring’ari’ katika gauni lililoshonwa kutokana na vipande vya magunia.
Katika ukurasa wake wa Instragram amekuwa akiwauliza mashabiki wake iwapo wanakubaliana au kupinga gauni hilo, majibu yao yamekuwa ni mengi mno – ya wale wanaokubaliana na kivazi hicho na wale wanaokipinga

Bella kufunga mwaka na Koffi, Dar Live


BELAKING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’.
Na Mwandishi Wetu
KING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kufunga mwaka (Desemba 31) na wimbo alioufanya na mkongwe wa muziki kutoka Kongo (DRC), Koffi Olomide uitwao Acha Kabisa, ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Akizungumza na mtandao huu, Bella anayetamba na Wimbo wa Nashindwa alisema usiku huo mashabiki watafunga mwaka kwa kuimba na kucheza ngoma zake zote kali kama vile Nani Kama Mama, Nakuhitaji, Msaliti, Nashindwa, Amerudi na nyingine kibao.
“Usiku huo nitafunga mwaka na kufungua mwaka mwingine nikiwa na bendi yangu ya Malaika Music huku tukitoa sapraiz kwa mashabiki wetu wote, pia kwa mara ya kwanza nitawaonjesha Wimbo wa Acha Kabisa niliofanya na Koffi Olomide pamoja na kutambulisha wimbo wangu mpya mwingine,” alisema Bella.
Mashabiki pia wategemee kupata sebene la aina yake kutoka kwa Malaika itakayokuwa na vichwa kama Adaya, Petit Mauzo, Pilu, Mico Bella, Chesco Vuvuzela, Yanick Soslo, Babu Bomba, Kadogoo Machine na wengine wengine wengi.
5_5Baada ya kufunga mwaka, katika Sikukuu ya Mwaka Mpya (Januari 1), bendi kongwe ya muziki wa Dansi, The African Stars ‘Twanga Pepeta’ ikiongozwa na Ali Chocky itakuwa na kazi moja ya kulishambulia jukwaa kwa kutoa sebene la kisasa.
Akizungumzia shoo ya kufungua mwaka, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa siku hiyo pazia la burudani litafunguliwa mapema kuanzia asubuhi kwa kutoa nafasi kwa watoto wote kusherehekea kuukaribisha mwaka mpya.
“Tutakuwa na kundi linalotikisa kunako miondoko ya sarakasi na mazingaombwe kwa watoto la Masai Warriors ambapo watatoa burudani zote bila kusahau watoto wote wataburudika na michezo mingi kama vile kuogelea, kuteleza, kubembea pamoja na kucheza ndani ya ndege maalum,” alisema Mbizo

Monday, December 21, 2015

A-Z aliyechinja mpenzi, watoto


IMG_8393
Mtoto baada ya kufanyiwa unyama huo.
Na Stephano Mango, SONGEA
MAJONZI! Bado ni tukio baya sana kutokea katika Kijiji cha Kikunja, Kata ya Ndongosi, Wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma ambapo mkazi wa kijiji hicho, Amani Hyela (42), anadaiwa kuwaua kwa kuwachinja kwa panga mpenzi wake, Ester na watoto wake wawili kisa kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Tukio hilo la kutisha lilijiri saa saba usiku wa Novemba 28, mwaka huu ambapo Amani anadaiwa kuwaua watu hao kwa kuwachinja na kuwakata na panga sehemu mbalimbali za miili yao na baadaye yeye kujijeruhi kwa kujikata shingoni na kujisababishia majeraha makubwa.
Kama ada ya Gazeti la Uwazi, mara baada ya kupata taarifa za ukatili huo lilifika eneo la tukio na kujikusanyia maelezo kutoka kwa mashuhuda na majirani wa eneo hilo.
“Mimi ni jirani wa marehemu Ester, siku hiyo usiku nilishtuliwa na kelele za watu. Nikatoka nje na kubaini kuwa, kelele hizo zilikuwa zikitokea kwenye nyumba hii. Kufika nikakuta watu wengi, mtuhumiwa yuko chini anavuja damu.
“Niliulizia kulikoni, nikaambiwa Amani amevamia nyumbani hapo na kumchinja Ester na watoto wake wote. Nilishangaa sana. Ester nilimwona mchana wake, alikuwa wa afya njema kabisa. Huu ni ukatili. Dunia ya sasa unyama umeongezeka sana. Si Tanzania tu. Kila mahali unyama, ukatili,” alisema jirani mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
IMG_8387
Mama akiwa amelala chini baada ya kufanyiwa kitendo hicho cha kinyama.
Shakira Moyo, mkazi wa kijiji hicho na mama mzazi wa marehemu Ester aliliambia gazeti hili kuwa, ni unyama mkubwa ambao haujawahi kutokea kwenye kijiji hicho na kwamba anamfahamu Amani ambaye ni mlalamikiwa.
Shakira alisema mauaji hayo yamemuumiza sana kwa vile yamempotezea mwanaye na wajukuu wawili ambao kimsingi hawana hatia yoyote katika wivu wa kimapenzi wa wazazi wao lakini wamekatishwa uhai wao.
Alisema kuwa marehemu Ester alikuwa na watoto wawili ambao walizaliwa kwa baba tofauti (si Amani) lakini kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Ester akawa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume huyo.
“Ester na Amani waliishi kama mume na mke na baadaye waliachana kufuatia Ester kusema kuwa ameokoka na kwamba hataki tena masuala ya mapenzi (nje ya ndoa) jambo ambalo lilipingwa na mwanaume,” alisema Shakira.
picha2
Mtuhumiwa akiwa amefungwa kamba.
Aliongeza kuwa, kitendo hicho ndicho kilichomfanya Amani kuamua kuchukua uamuzi huo uliosababisha vifo vya watu watatu na yeye mwenyewe kujijeruhi ambapo pia alinusurika kifo kutoka kwa wananchi wenye hasira.
“Inaonekana Amani aliamini Ester anamkataa kwa kuwa ana mwanaume mwingine ndiyo maana aliona bora amtoe uhai na kuwamaliza na watoto na yeye ajiue. Naamini amejijeruhi lengo lilikuwa kujiua,” alisema mwanamke huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, ACP Mihayo Msikhela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
IMG_8412Alisema siku ya tukio, baada ya taarifa kufika kituoni, polisi walikwenda eneo husika na kukuta watu hao wameshafariki dunia huku mtuhumiwa akiwa amejichinja koo akiwa amefungwa mikono kwa waya.
Alisema mtuhumiwa akiwa anavuja damu, alikimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ambako amelazwa akipatiwa matibabu huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Dunia katili



IMG_0969Mtoto Sabrina akiwa na majeraha usoni baada ya kumwagiwa maji ya moto na jirani kisa TV.
Na Makongoro Oging’
UBINADAMU umeisha! Ni ajabu lakini ni kweli imetokea! Mtoto Sabrina (7), mkazi wa Tabata Msimbazi, Dar anakabiliwa na maumivu makali kufuatia majeraha yaliyotokana na kumwagiwa maji ya moto na mwanamke anayesemekana ni jirani yao.
Tukio hilo la kushangaza lilijiri saa sita mchana wa Desemba 6, mwaka huu wakati mtoto huyo alipokuwa akiangalia kupitia dirishani, kipindi cha watoto kilichokuwa hewani runingani katika nyumba ya jirani yao huyo (jina tunalihifadhi kwa sasa) ambaye hapendi watoto wa majirani zake waende kwake.
Akizungumza na mwandishi wetu wiki iliyopita nyumbani kwake, Tabata jijini Dar, mama mzazi wa mtoto huyo, Mariam Athuman alisema siku ya tukio, Sabrina alikuwa akicheza nje ya nyumba kisha akaenda kwa jirani huyo kuangalia kipindi cha watoto.
IMG_0973Sabrina akiwa na mama yake mzazi
“Nikiwa nyumbani, alikuja mtoto mmoja akaniambia Sabrina amemwagiwa maji ya moto akiangalia tivii kwa jirani. Inasemekana mara ya kwanza alianza kumwagiwa maji ya baridi, akakimbia lakini baadaye akarudi tena.
“Huyo mtoto aliyeleta taarifa alisema mtu aliyefanya unyama huo aliagizwa na shangazi yake ambaye anaishi naye. Alipewa maji ya moto, akaambiwa ammwagie usoni Sabrina.
“Wakati naelekea eneo la tukio nilikutana na mwanangu akitembea kwa shida. Alikuwa haoni vizuri huku amebabuka uso. Nilimkimbiza kwenye Zahanati ya Tabata ambako walimsafisha uso kwa dawa kisha wakaniandikia nyingine za kununua.
“Baada ya hapo, nikaenda Kituo Kidogo cha Polisi Tabata. Pale nilifungua kesi kwa jalada namba TBT/RB/7418/2015 na jalada la uchunguzi TBT/IB/3835/2015.
“Polisi walimfuata aliyedaiwa kutumwa na shangazi yake ambapo alikiri kufanya tukio hilo. Polisi walimfuata shangazi huyo na kumchukua hadi kituoni, akawekwa mahabusu, mimi nikaondoka.
IMG_0970“Cha ajabu ni kwamba, baada ya kufika nyumbani, kama dakika ishirini mbele, nilimwona mtuhumiwa na shangazi yake wamerudi. Hatukujua sababu ya kuachiwa mapema kiasi hicho. Hii dunia ni katili sana,” alisema mama huyo huku akitokwa machozi.
Wakazi wa eneo hilo wameiomba serikali imchukulie hatua kali mwanamke huyo aliyetoa maagizo ya kufanyika kwa ukatili huo.
Uwazi lilifika kituo hicho cha polisi na kuuliza kisa mtoto huyo kuchomwa kwa maji ya moto lakini hakuna askari aliyekuwa tayari kutoa ushirikiano kuhusu kuachiwa kwa mtuhumiwa muda huohuo kama mlalamikaji alivyosema huku mkuu wa kituo akisemekana kuwa nje ya kituo.

Mwanamke wa unga jela miaka 20


madawaAnna Gemanist Mboya.
Na Makongoro Oging’
Mrembo wa madawa ya kulevya ‘unga’, Anna Gemanist Mboya mkazi wa Kijitonyama, Kinondoni jijini Dar amefungwa jela miaka 20 na kupigwa faini ya shilingi milioni 148, fedha anazotakiwa kuzilipa mara atakapomaliza kifungo.
Mrembo huyo ambaye ni mfanyabiashara, amefungwa Desemba, Mosi, mwaka huu mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Wilfrida Koroso kwa kosa la kusafirisha madawa ya kulevya.
Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini, SACP Godfrey Nzowa (pichani) amethibitisha kuhukumiwa kwa mrembo huyo na ameipongeza mahakama kwa kasi ya kuendesha kesi nyingi za madawa ya kulevya na kuzitolea hukumu.
Kwa mujibu wa Kamanda Nzowa, Anna alikamatwa Januari 2, mwaka 2011 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kikosi kazi (task force) kilichopo katika kiwanja hicho.
awa“Nawaomba wananchi waendelee kuwafichua wahusika wa madawa ya kulevya ili waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria na kuokoa taifa letu na biashara hii haramu,” alisema Nzowa.
TUMIA LIKIZO HII KUJIANDAA VIZURI
NAFAHAMU kabisa kuwa

Wednesday, November 25, 2015

ona makonda alivyo kuwa ana masiala

https://youtu.be/rZBbKClUP_Q

Mtazamo wa Kisheria wa Sakata la Mkuu wa Wilaya Kuwasweka Rumande Maofisa Ardhi.........Hapa Kuna Video Pia ya DC Makonda Akitoa Sababu za Kuwatia Ndani


Na. Julius Mtatiro,
Nilipo- post juu ya jambo hilo mjadala mkubwa wa wananchi umekuwa ni kutaka kujua sheria inaelekeza nini kwa mamlaka ya wakuu wa wilaya. Kwa uelewa wangu wa shahada ya kwanza ya sheria nimeona niwawekee hapa ufafanuzi wa kisheria kwa ajili ya faida yenu na mjadala mwingine tena.

Rais Magufuli Afuta sherehe za Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Kitaifa......Aagiza Fedha za Maandalizi ya Sherehe Hizo Zikanunulie Dawa za Waathirika


Rais John Magufuli amesitisha  maadhimisho ya siku ya Ukimwi kitaifa ambayo yalikuwa yafunguliwe mkoani Singida jana na kufikia kilele chake Desemba mosi mwaka huu mjini humo.

Badala yake Rais Dk Magufuli ameagiza fedha zote ambazo zilitengwa na serikali pamoja na wahisani mbalimbali kwaajili ya maadhimisho hayo zielekezwe kununua dawa kwaajili ya waathirika wa Ukimwi na  vitendanishi.

Akizungumza na moja kwa moja na Televisheni ya Taifa (TBC), Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk Fatma Mrisho, amesema serikali imetoa agizo hilo jana wakati tayari mkuu wa Mkoa wa Singida akiwa ameshafungua maonesho ya maadhimisho hayo.

“Serikali imesitisha maadhimisho ya mwaka huu Singida na badala yake fedha zilizopangwa kwaajili ya maadhimisho ziende zikanunue dawa za virusi vya Ukimwi, dawa za kudhibiti maambukizi ya ukimwi na vitenganishi,” amesema Mrisho.

Dk Mrisho amesema kuwa tayari taarifa za kusitisha maadhimisho hayo zimesha wafikia washiriki na wale walio kuwa njiani kuelekea Singida wamegeuza.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam juzi kabla ya sherehe hizo kusitishwa, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk Fatma Mrisho alisema maadhimisho ya mwaka huu yalikuwa yatanguliwe na maonesho ya wadau yatakayojumuisha huduma mbalimbali zikiwamo za utoaji elimu na burudani.

Dk Mrisho alisema huduma nyingine zilizopangwa kutolewa katika maadhimisho hayo ya wiki moja ni upimaji wa hiari wa watu zaidi ya 3,500  wanaoishi na virusi vya Ukimwi na utoaji ushauri nasaha, upimaji wa shingo ya uzazi, sukari, uzito, damu na kupata elimu itakayotolewa kupitia vikundi vya sanaa na burudani.

Maadhimisho ya mwaka huu yanachagizwa na kaulimbiu ya ‘Tanzania bila maambukizi mapya ya VVU, vifo vitokanavyo na Ukimwi na ubaguzi na unyanyapaa inazewekana.’

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Parseko Kone aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake hivi karibuni kuwa maadhimisho hayo yanatarajiwa kuanza Novemba 24 mwaka huu kwenye viwanja vya Peoples Club ambapo uzinduzi utakuwa Novemba 25 kabla ya kilele, Desemba mosi.

Hii ni mara ya tatu tangu Rais Dk Magufuli aingie madarakani kuzuia maadhimisho yanayogharimu fedha nyingi za  sherehe na fedha zake kuelekeza ikanunulie vifaa tiba mahospitalini.

Awali Rais aliagiza fedha zilizotengwa kwaajili ya hafla ya uzinduzi wa Bunge zaidi ya shilingi Milioni 225 ziende kununulia vitanda vya hospitali ya taifa Muhimbili.

Aidha Rais pia alisitisha maadhimisho ya siku ya Uhuru Desemba tisa mwaka huu na badala yake watu wafanye kazi katika maeneo yao ya kazi hasa usafi wa mazingira.

Monday, November 16, 2015

PENZI LA RAY, CHUCHU CHALI JOHARI MENO 32 NJE

Brighton Masalu

DAH! Imebuma! Lile penzi lililoziba masikio ya wengi kati ya waigizaji wakubwa Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans linadaiwa kuanguka chali kufuatia mume wa mwanamke huyo kutua nchini kimyakimya na hivyo kuwa wigo wa wawili hao kukutana kama zamani.
Staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu zaidi na Chuchu (jina lipo), ujio wa mwanaume huyo umemfanya Chuchu kuwa mbali na Ray hivyo penzi lao kuparaganyika.
“Yaani ngoma ilikuwa nzito. Ndiyo maana siku hizi Ray na Chuchu hawako beneti. Hata kwenye bethidei ya Wema (Novemba 1, 2015), Chuchu alifika, Ray hakutokea. Unajua Chuchu hadi sasa anasubiri uamuzi wa mwanaume huyo, ninavyojua penzi lake na Ray halipo tena,” alisema rafiki huyo.
Amani lilimtafuta Chuchu kupitia simu yake ya mkononi ili kusikia kauli yake, akasema:
“Jamani, hakuna kitu kama hicho, suala la mume wangu kuwa nchini sitaki kulizungumzia wala siyo matangazo. Ni suala langu na yeye, tafadhali sana naombeni mambo hayo muachane nayo. Ni ya kifamilia zaidi.”
Amani lilimtafuta na Ray angalau kuambulia chochote, lakini simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa. Akatumiwa meseji napo hakujibu.Kwa upande wa Johari aliyewahi kuwa mpenzi wa Ray alipotafutwa na kuelezewa juu ya hili aliishia kucheka tu

AUNT: SIHITAJI PEDESHEE, DANSA WANGU ANATOSHA

MAKUBWA! Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa wapo watu wanamcheka kuwa na uhusiano wa kimapenzi na dansa (Moze Iyobo) lakini ni bora aendelee kuwa naye kuliko kuwa na uhusiano na mtu mwenye pesa za kugawa hovyo (pedeshee) asiyekuwa na mapenzi ya dhati.

Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel akiwa na mpenzi wake Moze Iyobo.
Akizungumza na Amani, Aunt alisema kuwa aangalii hela hata kama wakilala njaa lakini kama kuna mapenzi ya kweli inatosha kabisa kuliko kuwa kwenye hela akaumizwa na kunyanyaswa.
“Acha niendelee kuwa na dansa wangu kuliko kuwa na pedeshee ambaye hana mapenzi ya dhati kwangu akaenda kuniumiza na nisione raha ya penzi, kwa Moo (Iyobo) nafurahia mapenzi na wala siyo pesa kwani hata njaa tunaweza kulala,” alisema Aunt.

SHAMSA: BORA NIFE KULIKO KURUDIANA NA MUME WANGU

Imelda Mtema

MAKUBWA!! Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Shamsa Ford ameibuka na kukataa katakata kurudiana na aliyekuwa mumewe, Dickson Matoke ‘Dick’ akisema kuwa kama watarudiana basi atakuwa ameshafariki dunia au bora afe kuliko kurudiana naye.
Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Shamsa Ford.
Shamsa aliyasema hayo juzikati baada ya kuulizwa na Amani kama ana mpango wa kurudiana na mumewe huyo ambapo alisema licha ya kuzaa mtoto mmoja (Terry) na mwanaume huyo, lakini katika maisha yake hafikirii kamwe kurudiana naye huku akasisitiza kuwa, kwa sasa ana maisha yake mengine.
“Mimi nirudiane na Dick? Labda niwe nimekufa na ni bora nife kuliko kurudiana na Dick. Ujue sasa hivi nina thamani kubwa zaidi na nipo na mtu ambaye ananipenda, nampenda,” alisema Shamsa.Hivi karibuni, Dick aliripotiwa na gazeti moja la Global akisema bado anampenda sana Shamsha na yuko tayari kurudiana naye baada ya kumwagana