NYOTA
wa kuigiza sauti za watu maarufu aliye pia mwigizaji wa sinema za
Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ wikiendi iliyopita alijikuta
akiaibika kwa kuzomewa na kupopolewa kwa chupa za maji na mashabiki wa Klabu ya Simba baada ya kuingia uwanjani na demu aliyevaa ‘kihasarahasara’.
Mwigizaji
wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’akiwa na mrembo
huyo.Ishu hiyo ilijiri Jumamosi ya Septemba 20, 2014 ndani ya Uwanja wa
Jamhuri mjini hapa wakati wa pambano kati ya Yanga na Mtibwa Sugar
katika Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo wenyeji walishinda 2-0
Steve
alitinga uwanjani saa 11:00 jioni akiwa na demu huyo mrefu
kwake,aliyetinga kipensi cha jinzi kifupi na tisheti ya njano na kijani
(zinazotumiwa na Yanga).
Wakati wawili hao wakipita kwenye jukwaa la mashabiki wa Simba, ndipo walipozomewa
na wengine kuwarushia chupa za maji kwa kile kilichodaiwa kuwa, demu
huyo alivunja maadili ya Kitanzania kwa kuvaa kihasara hadharani

No comments:
Post a Comment