
Marekani. Mwanamuziki Beyonce anafahamika kwa umahiri wake wa
kuteka vyombo vya vya habari wakati mwingine bila hata kufungua kinywa
chake. Ndoa yake, ujauzito wake na kuachia albamu kimyakimya ni mambo
ambayo yamewahi kuvunja rekodi za kuandikwa mara nyingi huku mwenyewe
akibaki kimya.
Katika mahojiano na Jarida la Bazaar, ‘supastaa’
huyo anafunguka kuhusu upande mwingine wa maisha yake katika muziki,
fasheni na familia.
Bazaar: Kama ukipewa nafasi ya kurudi utoto ni kitu gani utafanya?
Beyoncé: Nitaiamuru nafsi yangu ijiamini. Sasa
hivi nimefikia katika hatua ambayo sijali watu wengine wanasema nini juu
yangu. Nilipokuwa mdogo kila nilichofanya kwanza nilitaka kujua, je,
watu watanichukuliaje.
Bazaar: Mara nyingi umekuwa ukisema wewe ni mtu mwenye aibu, lakini katika kazi zako unaonekana unajiamini, hii ikoje?
Beyoncé: Sasa hivi sina aibu sana kama ilivyokuwa
zamani. Mimi ni mtu ninayependa zaidi kusikiliza kuliko kuongea ndiyo
maana naonekana kuwa na aibu. Ninajiamini, ninapenda ninachofanya na
ninajituma haswa.
Bazaar: Unawataja Diana Ross na Tina Turner kama unafuata nyayo zao, kitu gani hasa unakipenda kutoka kwao?
Beyoncé: Walikuwa ni wanawake waliojituma bila waoga. Kumbuka
pia
wanawake hawa waliofanikiwa kuchomoza katika jamii ambayo ilikuwa ikimdharau mtu mweusi.
Bazaar: Uko karibu sana na mdogo wako Solange, lakini aina ya maisha yenu ni tofauti, ni kitu gani kinawaunganisha?
Beyoncé: Kwanza kama ulivyosema Solange ni mdogo
wangu. Ninampenda sana na nafikiri tofauti zetu katika mambo
tunayoyapenda na kuamini ndiyo inayotuunganisha.
Bazaar: Ushauri gani mzuri ambao mama yako amewahi kukupa?
No comments:
Post a Comment