airport jogging

mavazi

aus521

aus9

Friday, December 5, 2014

Kibarua cha mama kumpa mwanawe 'Bangi'

 
Mama wa kijana anayeugua kifafa amekataa kumpa mwanawe wa kiume bangi kama matibabu inavyotakikana-kupitia moshi na mvuke. Mtoto huyo anapasawa kutumia Bangi kama dawa kupambana na ugonjwa wake wa Kifafa kwa maagizo ya daktari.
Liam McKnight mwenye umri wa miaka sita napenda kucheza na ndiye wa kwanza kila mara kukimbia kuelekea mlangoni.Mamake mzazi,Mandy,anasema kuwa mwanawe anapenda kujua nani anawatembelea.
Familia hiyo ya McKnight inayoishi jijini Otawa nchini Canada ina wageni wengi wanaowatembelea-kutoka kwa wanachama wa kukindi cha densi anachoshiriki binti yao,na hata wauguzi wa kutamka,wa kunyosha viungo vya mwili,wataalam wa kusikiza-wote wanaomtembelea Liam.
Liam ana ugonjwa unaojulikana kama Dravet ambayo,ni aina kali sana ya kifafa.Afya yake hudhoofika mara kwa mara lakini baada ya kufanyiwa majaribio kadha wa kdha ya matibabu ya ugonjwa huo, anglau hali yake imeimarika kidogo.
Mamake Liam humpa mafuta ya Bangi, ambayo yemtolewa kwa sehemu changa sana ya mmea huo.
Mwezi Juni mwaka huu,siku kabla Liam kuanza kutumia mafuta hjayo ya Bangi,(iliyotengezwa kutoka kwa aina ya bangi yenye ufanisi) alizirai kama mara 67. Katika siku kumi zilizofuatia alizirai tu mara moja.

No comments:

Post a Comment