
Waziri
wa mashauri ya Nchi za kigeni wa Sudan Kusini Barnabas Marial Benjamin,
amepuuzilia mbali tahadhari iliotolewa kua taifa hilo changa limo
katika hatari ya kukumbwa na baa la njaa.
Afisa mmoja mkuu wa
umoja wa mataifa ambaye ndio mwanzo amefika Sudan Kusini kufanya kazi
kama naibu mshirikishi mkuu wa utoaji msaada wa dharura, Kyung-wha Kang,
amesema kuwa watu milioni mbili unusu wamo katika hatari ya kuangamizwa
na baa la njaa kwa sababu ya ukosefu wa chakula.Amesema hiyo ni kutokana na mapigano mapya na hali tete ya usalama nchini humo.
Aidha ameongeza kusema kuwa kuna matumaini ya muafaka wa amani kati ya Rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar, ambaye kufikia sasa hajakubali kuhudumu kama waziri mkuu mwenye mamlaka makubwa.

No comments:
Post a Comment