airport jogging

mavazi

aus521

aus9

Thursday, April 23, 2015

MWANAMKE ARUKA UKUTA, AIBA MASHUKA NA DEKI

aus9
Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Asha Saidi, hivi karibuni alikiona cha moto baada ya kufumwa akiiba mashuka na deki kwenye nyumba ya jirani yake.Tukio hilo lilitokea mtaa wa Mawenzi ambao mama huyu anaishi, inadawa aliruka ukuta na kukutwa na mama mwenye nyumba anayeitwa Zainabu akifanya uhalifu huo.
Asha Saidi akiwa na Deki aliyodaiwa kuiiba.
Ilidaiwa kuwa baada ya Zainabu kushuhudia tukio hili alipiga kelele za mwizi ndipo watu walipojitokeza na kumtaiti.Hata hivyo, wakati mwanamke huyo akiwa chini ya ulinzi wa raia, polisi walifika na kumtia nguvuni  na alipoulizwa sababu ya kuiba alijitetea.
“Jamani naomba mnisamehe ninaumwa na maisha yangu ni magumu, nasumbuliwa na Malaria hivyo niliona njia ya kujipatia matibabu ni hii kwani sikuwa na hela kabisa,” alisema Asha.

...Akiwa mikononi mwa polisi.
Wapangaji waliokuwa kwenye nyumba hiyo walisema kuwa kabla ya tukio hilo jana yake kulitokea wizi wa simu ambayo ilisababisha mtafaruku baina ya wapangaji lakini hawakumpata mwizi hivyo wakadai huenda Asha alihusika.Hata hivyo, polisi waliofika eneo la tukio walimchukua mwanamke huyo na kumpelekea kituoni kwa mahojiano zaidi

No comments:

Post a Comment