MAJANGA! Mwanadada Elizabeth Kinyami mkazi wa Kibaha
mkoani Pwani amedaiwa kumtoroka mumewe, Robert Nassor na kwenda Tanga
kuchumbiwa na mwanaume mwingine, Risasi Mchanganyiko limetonywa.

Inadaiwa kuwa baada ya kuishi kama mke na mume kwa miaka miwili, msichana huyo alimwambia Robert kuwa amepata chuo cha kusoma mjini Tanga, ambapo mwanaume alikubali na kumsaidia ili aendelee na masomo.
Muhula wa masomo ulipoisha, Robert alimtumia nauli ili arejee, lakini katika hali ya kushangaza, hakurudi licha ya kutumiwa mara tatu, kabla ya mwanaume huyo kuamua kumfuata na alipofika huko ndipo alipobaini kuwa alikuwa akiishi na mwanaume mwingine.

Kwa upande wake, Elizabeth alisema madai hayo siyo ya kweli, kwani Robert anauelewa ukweli wa suala lake, bali yeye aliwahi kumfumania mwenzake mara nyingi.“Kuhusu hili suala, yeye analijua mwanzo mwisho, nitamtafuta ili tuzungumze,” alisema mwanamke huyo.
Elizabeth Kinyami anayedaiwa kumtoroka mumewe.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini Robert alifiwa na mkewe wa kwanza
ambaye alizaa naye watoto wawili, lakini wakati akiwa naye, alikuwa
akichepuka na Elizabeth, hivyo baada ya mwenzake kutangulia mbele ya
haki, alimchukua mchepuko wake na kuishi naye kinyumba.Inadaiwa kuwa baada ya kuishi kama mke na mume kwa miaka miwili, msichana huyo alimwambia Robert kuwa amepata chuo cha kusoma mjini Tanga, ambapo mwanaume alikubali na kumsaidia ili aendelee na masomo.
Muhula wa masomo ulipoisha, Robert alimtumia nauli ili arejee, lakini katika hali ya kushangaza, hakurudi licha ya kutumiwa mara tatu, kabla ya mwanaume huyo kuamua kumfuata na alipofika huko ndipo alipobaini kuwa alikuwa akiishi na mwanaume mwingine.
Mume anayedaiwa kutorokwa na mkewe.
“Ni kweli Eliza ni mke wangu, nimemsaidia kumtafutia chuo lakini
ukweli ni kwamba alikuwa ananilaghai, kumbe alikuwa na mambo yake,
nimemgharamikia sana ikiwemo mawigi, mikoba na vitu vingine akidai
anaenda chuo Tanga, kumbe alikuwa na mwanaume mwingine,” alisema Robert
alipotakiwa kutoa ufafanuzi.Kwa upande wake, Elizabeth alisema madai hayo siyo ya kweli, kwani Robert anauelewa ukweli wa suala lake, bali yeye aliwahi kumfumania mwenzake mara nyingi.“Kuhusu hili suala, yeye analijua mwanzo mwisho, nitamtafuta ili tuzungumze,” alisema mwanamke huyo.

No comments:
Post a Comment