
Salma Jabu maarufu kama Nisha.
SALMA Jabu maarufu kama Nisha amelazimika kuhama
mtaa aliokuwa akiishi mwanzo huko Kijitonyama, akiwakimbia vibaka baada
ya hivi karibuni kumuibia vifaa ndani ya gari lake.Nyota huyo wa filamu ameamua kuhamia mitaa ya Mbezi Beach baada ya kuhisi huenda vibaka hao wanaweza kurudi na kumfanyia uhalifu mbaya zaidi ya ule wa kuligeuza gari lake gofu kwa kuiba kila kitu cha ndani.
“Tangu nilipoibiwa sikuwa na amani kabisa ya kuendelea kuishi pale Kijitonyama, ndiyo maana nikaamua kuhama na kweli nimepata amani ya moyo, naendelea vizuri na maisha japokuwa natumia teksi kwa kuwa sina gari,” alisema Nisha
No comments:
Post a Comment