airport jogging

mavazi

aus521

aus9

Tuesday, September 8, 2015

RAIS KIKWETE AWAPA POLE MAJERUHI YA MSONGAMANO WA WANANCHI BAADA YA MKUTANO WA KAMPENI KATIKA UWANJA WA JAMHURI MJINI MOROGORO JANA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika msongamano mkubwa uliotokea katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni wa CCM katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015. Watu wawili walipoteza maisha, akiwemo mvulana wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Abdallah na mwanamama Grace George (42), ambapo jumla ya watu 17 walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini hapo. Hadi jioni hii majeruhi saba walikuwa wameruhusiwa
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kaimu Mganga Mku wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Samson Tarimo alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mweka Hazina wa CCM mkoa wa Morogoro Ndg. Hassan BAntu alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015.
 Mmoja wa majeruhi Bw. Kokoliko Ramadhani akiwa kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo
 Rais Kikwete akimpa pole  mmoja wa majeruhi Bw. Kokoliko Ramadhani akiwa kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo
 Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimpa pole  mmoja wa majeruhi Bi Flora Maduka akiwa kitandani pake hospitalini hapo baad ya kujeruhiwa katika msongamano huo
 Rais Kikwete akimpa pole  mmoja wa majeruhi Bi. Jalia Mohamed akiwa kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo
 Rais Kikwete akiendelea kutoa pole kwa majeruhi
 "Pole sana...." Rais Kikwete akimfariji mmoja wa majeruhi

 Rais Kikwete alitumia wasaa huo kuwapa pole wagonjwa wengine waliokuwa wamelazwa wodi moja na majeruhi hao. Hapa anamfariji mtoto aliyeungua kwa moto
  Rais Kikwete alitumia wasaa huo kuwapa pole wagonjwa wengine waliokuwa wamelazwa wodi moja na majeruhi hao. Hapa anamfariji mtoto aliyevunjika mguu wakati akicheza kwenye mti
Rais Kikwete akimpa pole mvulana ambaye aligongwa na gari wakati akielekea kumsikiliza mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana 
Rais Kikwete alipata fursa ya kutembelea wodi ya watoto na kuwapa pole kwa kuumwa kwao
Rais Kikwete akiongea na wanafunzi waliokuwepo hospitalini hapo kumtembelea mgonjwa
Rais Kikwete alizongwa na wananchi waliokuwa na hamu ya kuongea naye 
Rais Kikwete akitoa mapendekezo ya kupanua hospitali hiyo ambayo ina eneo kubwa lakini majengo machache ya chini. Alipendekeza uongozi wa hospitali na mkoa ubuni namna ya kuipanua kwa kujenga majengo ya ghorofa ili kuwepo na wodi na sehemu nyingi zaidi za huduma.
Mwishoni Rais Kikwete aliongea na wanahabari wa kutoka vyombo mbalimbali na kueleza masikitiko yake kwa yaliyotokea jana Uwanja wa Jamhuri baada ya mkutano wa kampeni kumalizika.
Rais Jakaya Kikwete akiongea na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya baada ya kuwajulia hali majeruhi wa msongamano baada ya mkutano wa kampeni uwanja wa Jamhuri Morogoro jana. PICHA NA IKULU

MAGUFULI KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI KISAYANSI


 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akisoma bango la vijana wafanya biashara ndogo ndogo wa eneo la Dumila maarufu kama Feri wakati akielekea mkoani Tanga ikiwa muendelezo wa mikutano ya kampeni za CCM .
 Wananchi wanaoishi eneo la Dumila wakimsikiliza Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuliakimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Mvomero Sadiq Murad kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Mvomero, mkoani Morogoro.
 Wanachama wa CCM wakionyesha mabango ya mgombea wao wa Ubunge Ndugu Sadiq Murad kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kihalawa,Turiani mkoani Morogoro.
 Mzee Yusuph Makamba akihutubia wakazi wa Turiani mkoani Morogoro kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa CCM pamoja na sera za CCM kwa wananchi wa Turiani.
 Kikundi cha akina mama wahamasishaji kikiingia uwanjani kwenye eneo la mkutano wa kampeni za CCM Turiani ambapo Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli alihutubia.
 Wazee wa Turiani wakimsikiliza kwa makini Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuliakihutubia wakazi wa Turiani mkoani Morogoro na kuwaambia atahakikisha migogoro ya ardhi inamalizika na kuileta jamii kuishi kwa amani na upendo.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuliambapo aliwaambia wananchi hao ataunda baraza dogo la mawaziri lakini pia atahakikisha barabara zinakamilika kwa kiwango cha Lami.
 Wakazi wa Turiani mkoani Morogoro wakimsikiliza Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufulikwenye mkutano wa kampeni.
 Wananchi wakiinua mikono kuonyesha kukubaliana na Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi ilani ya uchaguzi mgombea ubunge wa jimbo la Mvomero Ndugu Sadiq Murad.
 Mama akifurahia jambo kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Turiani mkoani Morogoro.
 Wakazi wa Kwaluguru wakimsubiri Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli afike na kuwasalimu wakazi hao.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge jimbo la KilindiOmari M. Kigua wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Kwaluguru.
 Wakazi wa kijiji cha Bandari kata ya Kimbe wakimsikiliza Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Wakazi wa Songe wakifurahia ujio wa Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Songe ambapo aliwaambia wananchi hao katika uongozi wake atasimamia haki kwa wananchi wote na kuhakiisha huduma zote za msingi zinapatikana.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Kibirashi
 Msafara wa Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli ukiwasili Kwediboma.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuliakihutubia wakazi wa Kwediboma.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli(katikati) akiwanadi Mbunge wa Handeni Mjini Dk. Abdallah Kigoda (kulia) na Mgombea wa Ubunge Jimbo la Handeni Vijijini Ndugu Mboni Mhita kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uliofanyika kwenye uwanja wa Azimio Center.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgombea wa ubunge jimbo la Handeni mjini Dk. Abdallaha Kigoda.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Handeni Vijijini Ndugu Mboni Mhita.
Wananchi wa Handeni wakishangilia jambo kwenye mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Azimio Center mkoani Tanga.

UONGOZI WA CHADEMA WILAYA YA KILOSA WAJIUNGA NA CCM

Viongozi watatu wa Chadema wilaya ya Kilosa na mwanachama mmoja wametangaza kujiunga rasmi na CCM baada ya kuchoshwa na siasa za Chadema ambazo wameona hazina haki.
 Viongozi hao waliohamia CCM ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kilosa Ndugu Selemani Simba, Katibu wa Chadema wilaya hiyo Ndugu Ibrahim Abdallah Selemani, aliyekuwa Katibu wa Jimbo la Kilosa Kati Mussa Ngongo na aliyejitambulisha kama mwanachama kiherehere wa Chadema Bi.Oliver Mollel.
Viongozi hao walitangaza kukihama chama cha Chadema kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM mbele ya mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Kilosa town.

MAGUFULI AITEKA MOROGORO MKUTANO WAKE WAWEKA HISTORIA

 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa Jamhuri tayari kuhutubia wakazi wa Morogoro mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
 Wananchi wakimkaribisha Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
 Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakifurahia ujio wa mgombea wa Urais wa CCM Dk.John Pombe Magufuli.
 Mwenyekiti wa CCM ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Ndugu Innocent Kalogeresi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Alhaji Abdalla Bulembo kwenye mkutano wa kampeni za CCM  uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri.
 Mwenyekiti wa CCM ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Ndugu Innocent Kalogeresi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Alhaji Abdalla Bulembo kwenye mkutano wa kampeni za CCM  uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri.
 Wananchi wakiwafurahia wasanii wa Tanzania wanaounda umoja unaofahamika kama Mama Ongea na Mwanao.

 Mzee Yusuph Makamba akisalimiana na Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Jamhuri, kulia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
 Wananchi wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kwenye mkutano wa Kampeni
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Alhaji Abdallah Bulembo akiwahutubia wakazi wa Morogoro mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa Mgombea wa CCM amejitosheleza kuongoza nchi yetu.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakazi wa Morogoro mjini ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa mchakato wa kumpata Mgombea wa Urais ulikuwa wa haki na kila mjumbe alipiga kura.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakazi wa Morogoro mjini ambapo aliwaambia wananchi hao hana mashaka na mgombea urais wa CCM na kuwataka wananchi  hao kumpigia kura siku ya oktoba 25.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akipanda ngazi za jukwaa kwa kukimbia mbio tayari kwa kuhutubia wakazi wa Morogoro mjini.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Morogoro mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri.


 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika uwanja wa Jahmuri.
 Mzee Yusuph Makamba akipanda ngazi za jukwaa tayari kuhutubia wakazi wa mji wa Morogoro.
 Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Yusuph Makamba akizungumza na wananchi wa mkoa wa Morogoro wakati wa mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa urais kupitia chama hicho Dk. John Pombe Magufuli uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
 Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Yusuph Makamba akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa urais kupitia chama hicho Dk. John Pombe Magufuli uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments:

Post a Comment