airport jogging

mavazi

aus521

aus9

Tuesday, September 1, 2015

UCHAGUZI 2015, NI MWAKA WA TABU


Mgombea urais wa Ukawa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.
Na Mwandishi Wetu
NDIYO lugha nyepesi kutamkika katika kipindi hiki ambacho nchi iko kwenye safari ya kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.Vyama vikubwa ni viwili, Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliomsimamisha Dk. John Magufuli na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliomsimamisha Edward Lowassa.
Mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, kwa sasa maeneo mengi ya kikazi yametawaliwa na habari za siasa kiasi kwamba, baadhi ya huduma zimekuwa chini.
James Mutumbwi, abiria aliyeshukia Kituo cha Mabasi ya Mikoani, Dar (UBT) juzi akitokea Arusha alisikika akisema:
“Huu ni mwaka wa tabu. Safari nzima ni siasa tu. Hakuna kusikilizana. Abiria wenyewe hata hawajuani nani yuko chama gani, wao wanatangaza wazi vyama vyao, hawajui kama ni hatari?
“Afadhali
uchaguzi upite tujue moja. Siku hizi hata watoto wanaangalia taarifa ya habari na kujaza sebule, ukiwaambia wajisomee hawataki,” alisema Mutumbwi.Baadhi ya wafanyabiashara kwenye Soko la Magomeni Mapipa, Dar nao walilalamikia siasa kuingizwa kwenye maeneo ambayo si ya lazima au hayahusiani na mambo hayo.
“Wengine ni wateja wetu wa kila siku. Sasa cha kushangaza leo wanakuja na kutuuliza sisi tuko upande gani wa vyama. Mmoja alisema kama sipo chama anachokishabikia yeye haniungishi tena samaki. Kwa kweli nilimwambia hata asiponiungisha yeye, wataniungisha hao wenye chama kinachofanana na changu,” alisema mama Mushi mfanyabiashara katika soko hilo.
Nguvu ya ushindani ni kubwa sana kiasi kwamba, maisha ya mtaani ni ya upinzani pia. Tabu ni pale majirani wanapotumbuliana macho kisa siasa za mwaka huu.Juzi maeneo ya Manzese Tip Top, Dar, baadhi ya watu waliobainika ni wafuasi wa CCM na Chadema walitukanana matusi hadharani kisa kikiwa ni kila upande kujitapa kwamba wakati wa kampeni za uzinduzi kwenye Viwanja vya Jangwani, upande wao ulifunika.
Nje ya Kanisa la Romani Katoliki, Parokia ya Manzese, juzi Jumapili, baadhi ya waumini walitumia fursa ya kukutana kwao baada ya ibada ya kwanza kwisha na kuzungumzia siasa ya mwaka huu.
“Mimi nimewaambia watoto wangu wasishabikie mitaani. Wasubiri Oktoba wakapige kura. Unajua ushabiki wa mitaani si mzuri unaweza kusababisha ugomvi,” alisema muumini mmoja.
“Ni kweli, mimi nawaogopa sana vijana ambao hawana cha kupoteza. Hawa ndiyo wabaya kwa siasa za ugomvi. Vijana ambao hawana cha kupoteza ndiyo wanaoandamana kufanya fujo, ndiyo wanaoweza kufanya lolote kwani wanakoishi hawaangiliwi na mtu yeyote katika familia. Yaani mwaka huu, tumwombe Mungu kwa ajili ya amani ya taifa,” alisema muumini mwingine.

No comments:

Post a Comment