Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini, Hamis Mwinjuma maarufu kama MwanaFA.
Na Mwandishi WetuMKONGWE wa muziki wa kizazi kipya nchini, Hamis Mwinjuma maarufu kama MwanaFA, amesema pamoja na uchaguzi mkuu wa mwaka huu kuwa na msisimko mkubwa kuliko wakati mwingine wowote, haamini kama kutakuwa na vurugu.
Alisema hamasa iliyooneshwa na vijana mwaka huu ni ishara ya watu kukua kiakili na kutambua wajibu na haki zao, akidai hicho ni kitu kizuri kwa sababu kinatoa ishara kwa viongozi kuelewa kuwa Watanzania wa sasa siyo wale wa zamani.
“Hamasa haimaanishi fujo, Watanzania wote wanataka amani na ninaamini kabisa kuwa hakuna kijana atakayeanzisha vurugu kwa ajili ya matokeo ya uchaguzi, ninachokiona ni somo kwa viongozi kuwa waelewe wanawaongoza watu wanaojitambua, ambao wanaonesha hisia zao halisi,” alisema.

No comments:
Post a Comment