Esma Abdul akiwa na aliyekuwa mumewe Hamad Manungwa ‘Petit man’.
Na Imelda Mtema Dada wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond,’ Esma Abdul amerudisha mahaba na aliyekuwa mumewe, Hamad Manungwa ‘Petit man’ baada ya kudaiwa kutengana, tena kwa talaka tatu.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, mpashaji wetu alisema Esma na Petit kwa sasa wako katika mapenzi motomoto na hivi karibuni walionekana pamoja wakiwa nyumbani kwa Wema Sepetu na mtoto wao, Taraj.
Gazeti hili lilimtafuta mwanaume huyo na kumuuliza juu ya ubuyu huo ambapo alisema; “Bado tuko kwenye maongezi, lakini sisi ni wazazi na hata juzi tulimpeleka mtoto kwa bibi yake ambaye ni Wema amuone, maana yule ni mtu muhimu sana kwangu,” alisema Petit man

No comments:
Post a Comment