Mwezi Novemba mwaka huu mwimbaji Davido ambaye alivuma na album ya Omo Baba Olowo (Mtoto wa Tajiri) alijirusha na wasichana kadhaa wakati wa bethidei yake na mmoja wao alikuwa Masogane na baadaye zikaenea habari kwamba alikuwa mjamzito akitegemewa kumzalia Davido mtoto wa pili, lakini habari hizo baadaye zikakanushwa.
Kitu cha ajabu ni kwamba Masogange alianza kuweka na kufuta ujumbe mbalimbali kwenye mtandao ukionyesha alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Tekno kwa kula naye bata katika hoteli moja nchini Afrika Kusini.
Tekno
naye alianza kutuma ujumbe kama huo, jambo lililowafanya mashabiki wake
kuamini alikuwa na uhusiano na msichana huyo. Hata hivyo, mwimbaji huyo
ameufuta ujumbe wote huo katika ukurasa wake

No comments:
Post a Comment