airport jogging

mavazi

aus521

aus9

Tuesday, May 31, 2016

Prezzo amfuata Gigy Bongo!

Prezzo
IMEVUJA! Kumbe rapa mwenye jina kubwa Afrika Mashariki, Jackson Makini ‘Prezzo’moja ya ishu zilizomleta Bongo ni pamoja na kukutana na muuza nyago kwenye Video za Kibongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’.
Gigy Money
Akichonga na mtandao huu, Prezzo aliyewahi kubamba na Ngoma ya Nipe Nikupe akimshirikisha staa wa Bongo Fleva, Ambwene Yessaya ‘AY’ alisema kuwa, Gigy ni msichana ambaye amekuwa akimsikia siku za hivi karibuni Wakenya wakimzungumzia hasa juu ya vituko vyake jambo lililomfanya kuvutiwa kuonana naye.
“Gigy yuko hot mazee, nimemsikia sana Wakenya wakimzungumzia so nipo katika mpango wa kuonana naye, si unajua mimi nina mambo mengi, reality show na vitu vingine private,” alisema Prezzo. Gigy Money aliponyetishiwa ishu hiyo alifurahia jina lake kupaa hadi Kenya.

No comments:

Post a Comment