Mwandishi wetu, Amani
DAR ES SALAAM: “Msongo wa
mawazo ni tatizo kubwa duniani linalotokana na kusheheni kwa mawazo ya
kila wakati, husasan kuhusu maisha au afya. Kwa hiyo anachofanya Diamond
kwa baba yake ni sawa na kumuua kwa sababu ya kumsababishia msongo,”
ndivyo alivyosema daktari Rweyemamu wa hospitali moja ya jijini Dar.
Daktari Rweyemamu alizungumza na Amani
hivi karibuni kufuatia habari zinazoandikwa na Magazeti Pendwa ya Global
Publishers kuhusu nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwamba
amemtelekeza baba yake, Abdul Juma.
AZUNGUMZIA HISTORIA
“Nimekuwa nikisoma habari mbalimbali
kwenye Magazeti Pendwa ya Global, lakini hili la Diamond kumtelekeza
baba yake mimi naona lina mapana yake. Najua utetezi wa Diamond ni
kwamba, baba alimtelekeza mama yake (Sanura Kasim) yeye akiwa mtoto.
“Kwa hiyo malezi yote, ameyapata kwa
mama mpaka kufika kwenye kiwango cha mafanikio. Lakini pia nimewahi
kusoma kwamba, baba aliomba msamaha yaishe, atambulike kama baba lakini
mtoto akagoma.”
MAGONJWA YA BABA
“Kuna wakati nikasoma kwamba, yule mzee
anasumbuliwa na miguu, mara sijui ugonjwa wa kansa ya ngozi. Pia amekuwa
mtu wa kuumwa mara kwa mara.”
MSONGO WA MAWAZO
NI CHANZO
“Yule mzee atakuwa na magonjwa mengi,
hasa yanayotokana na msongo wa mawazo. Mawazo yake kwa sasa ni kitendo
cha kuona mafanikio ya mwanaye akilinganisha na maisha yake magumu bila
msaada.
“Binadamu yeyote, anapomwona mtu wake wa
karibu amefanikiwa na yeye hali duni lakini huyo aliyefanikiwa anaweza
kumsaidia yeye akaondokana na hali duni, lazima asumbuliwe na msongo.”
MIGOGORO, UGUMU
WA MAISHA
“Lakini pia migogoro inayotokea katika
familia, ni moja kati ya sababu zinazoweza kumpa mtu msongo wa mawazo,
hasa pale ambapo utaichukulia ‘serious’ kwa kuwa inagusa moja kwa moja
maisha yake. Ugumu wa maisha unachangia pia.”
MWILI UNAVYOATHIRIWA
NA MSONGO
“Moja ya sababu ambazo zinachangia kwa
kiasi kikubwa kuzorota kwa afya na kusababisha vifo vingi ni msongo wa
mawazo. Mwili unavyokutana na hali tofauti aidha kitu cha kutisha au
kinacholeta mawazo ndani ya muda mfupi na tofauti hiyo ikashindwa
kutambuliwa haraka na ubongo mfano pale unapokutana na jambo
usilolitegemea, basi mwili hutoa kichocheo kinachoitwa cortisol ambacho
kinamwagwa kwenye damu ili kuuandaa mwili aidha kupigana au kukikimbia
kitu hicho.
“Mapigo ya moyo huongezeka, mapafu
huchukua kiwango kikubwa cha hewa na mzunguko wa damu pia huongezeka na
baadhi ya sehemu za kinga huzidiwa na mzigo mkubwa hivyo kutoa nafasi
kwa viumbe adui kuushambulia mwili kirahisi.
“Msongo wa mawazo unapokuwa mkubwa siku
hadi siku ndipo kinga ya mwili inavyozidi kushindwa kubaini uwepo wa
kichocheo cha cortisol, msongo unapunguza makali ya kinga ya mwili,
hivyo matatizo ya afya huongezeka.”
UTAFITI
“Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na
World Health Organization, Shirika la Afya Duniani ‘WHO’, maradhi ya
moyo, akili, ugumba, ukosefu wa nguvu za kiume na vidonda vya tumbo, pia
yanacha-ngiwa na msongo wa mawazo.”
LAZIMA BABA
DIAMOND AWE HIVI
Kwa mujibu wa daktari huyo, lazima baba
Diamond wa sasa atakuwa amebadilika tabia, kwamba atakuwa mpole na siyo
mwenye furaha kwa muda mwingi.
“Kuishi kwa kubangaiza pesa za kula huku
akiwa anajua mwanaye anazo, tena mpaka zinamzidia, baba Diamond atakuwa
anamalizika polepole. Lazima kila akiamka, anasema; ‘mateso yote haya,
mwanangu yupo lakini hataki kunisaidia.”
WITO WAKE KWA DIAMOND
Daktari huyo alisema kuwa, anamtaka Diamond kurejesha moyo wake nyuma, amtunze baba yake ili amuokoe na kumalizika.
“Namtaka Diamond ajue kuwa,
anachomfanyia baba yake ni kumuua bila yeye kujua. Ukuta anaomuwekea
katika usaidizi unamfanya mzee huyo kunyemelewa na magonjwa ya moyo na
vidonda vya tumbo ambavyo kwa mazingira ya maisha yake yanaweza
kumsumbua kwani yanahitaji kipato kizuri.
No comments:
Post a Comment