airport jogging

mavazi

aus521

aus9

Wednesday, January 4, 2017

MTU mmoja amenusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa risasi na askari wa wanyamapori Sumbawanga


Mtu mmoja amenusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa risasi na kujeruhiwa mguu wa kulia na askari wa wanyamapori wa pori la Akiba la Uwanda kwa madai kuwa alikatisha kwenye hifadhi kinyume cha sheria.


Akizungumza na Channel ten majeruhi huyo, Salaganda Chela amesema ilikuwa jana saa tano asubuhi katika kijiji cha Legeza Kata ya Kipeta wilaya ya Sumbawanga alipigwa risasi katika nyumba ya jirani akinamama wakishuhudia.

Ndugu wa majeruhi wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro baina ya hifadhi ya Uwanda na vijiji vinavyoizunguka hifadhi hiyo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Kamishina Msaidizi wa Polisi, George Kyando amesema tayari askari anayetuhumiwa kumpiga risasi mwananchi amekamatwa na kumtaja kwa jina la Lemomo Miseyeke mfanyakazi wa hiafdhi ya Uwanda

No comments:

Post a Comment