airport jogging

mavazi

aus521

aus9

Wednesday, January 4, 2017

NAY ataja tofauti ya Diamond na Alikiba


Rapa Nay wa Mitego amefunguka na kuweka wazi kuwa katika wanamuziki watatu wakubwa Tanzania wazuri kwake yeye Alikiba atakuwa namba moja ila katika wanamuziki wakubwa watatu wafanyabiashara basi Diamond Platnumz atakuwa namba moja.Nay ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Sijiwezi', amesema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo cha EATV na kusema siku zote yeye amekuwa akimkubali sana Alikiba ingawa anatambua wazi mtaani kuna tetesi kuwa hawezi kufanya naye kazi kutokana na yeye kuwa na uswahiba na Diamond Platnumz.


"Watu wanajenga picha kuwa mimi na Alikiba siwezi kufanya naye kazi sababu tu ya uswahiba wangu na Diamond ni kweli Alikiba si mshikaji wangu lakini leo hii ukiuliza nikutajie wanamuziki watatu wazuri Tanzania wa kwanza nitamtaja Alikiba, lakini pia ukisema nitaje wasanii watatu wakubwa wafanyabiashara basi nitamtaja Diamond Platnumz" alisema Nay wa Mitego.

No comments:

Post a Comment